Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya ikiongozwa na Katibu wa Wilaya Ndg. Charles J. Seleman, imefanya ziara ya kukagua Miradi ya Ujenzi wa vyumba ya Madarasa unaotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea miradi 10 ya ujenzi wa vyumba ya madarasa katika shule za sekondari na vituo shikizi, miongoni mwa shule za sekondari zilizotembelewa ni pamoja na shule ya Sekondari Sangambi inayojengwa vyumba vya madarasa 11, Shule ya Sekondari Chokaa inayojengwa vyumba 2, Shule ya Sekondari Itewe yenye ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, Ujenzi wa vyumba 2 Shule ya Sekondari Makalla, Ujenzi wa vyumba 7 katika Shule ya Sekondari Kipoka na Maradi wa vyumba 3 katika sekondari ya Makongolosi.
Aidha kamati imetembelea Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa katika vituo shikizi, miongoni mwa vituo vilivyotembelewa ni Kituo Shikizi cha Mpaliji chenye ujenzi wa vyumba 2, kituo shikizi cha Mererani chenye ujenzi wa vyumba 4, Kituo shikizi cha Kalungu chenye ujenzi wa vyumba 3, pamoja na Kituo shikizi cha Machinjioni chenye ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa.
Akizungumza kwa niaba ya Mweyekiti wa CCM Wilaya, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Charles Seleman, ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa vyumba ya madarasa unaotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa wilaya walisema utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa unakwenda vizuri na kuutaka uongozi wa Halmashauri kuongeza kasi zaidi ili kukamilisha ujenzi wa vyumba kwa madarasa yaliyobaki.
Naye Mbunge wa Jimbo la Lupa - Chunya, Mh.Masache Njelu Kasaka ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa fedha pamoja na kazi nzuri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa fedha za UVIKO-19.
“Sisi leo tumekuja kama Kamati ya Siasa ya Chama CCM Wilaya tumeridhika na utekelezaji wa miradi hii ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani majengo haya yanaakisi fedha zilizotolewa, sisi kama wilaya tumeridhika na tulichokiona”.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Chama Cha Mpinduzi [CCM] wilaya ya Chunya Wakikagua Mradi wa Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Kipoka
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wakiendelea na Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi wa vyumba ya Madarasa unaotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.