Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kupitia chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chunya Bi .Ezelina Anyosisye Mwakasole amewataka wanawake wilayani Chunya kutowatenga watoto wakati wanapowalea kwani kufanya hivyo kunasababisha uonezi, ukandamizwaji kwa Watoto
Ameyasema hayo Jana tarehe 8 Machi 2023 katika maadhimisho ya siku ya wanawake wilayani Chunya
"Mnapowapangia kazi watoto muwapangie kwa usawa ikiwa ni kuchota maji mtoto wa kike na Wa kiume wote wakachote maji, ikiwa ni majukumu yanayohusu kupika Kuosha vyombo wote wafanye shughuli hizo kwanza kuwafundisha kazi wote bila kujali jinsia
Aidha Bi Mwakisole amewataka wanawake kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI kwani wameweza katika mapambano mengine mengi na wamefanikiwa katika mapambano hayo hivyo wakiamua wanaweza kutokomeza janga la UKIMWI
“Hebu tupige vita Sasa ukimwi usiendelee kututesatesa, Kama tumeweza kupambana kwenye Mambo mengine ikiwepo usawa katika Elimu, ajira na mambo mengine hivyo hata kwenye mapambano ya maambukizi tupambane ili tuepukane na maambukizi ya UKIMWI”
Katika hafla hiyo Mgeni Rasmi ametunuku vyeti vya pongezi kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali wilayani Chunya ambavyo vimeweza kurejesha mikopo waliyokopeshwa na Halmashauri hiyo kwa uaminifu huku wanachama wa vikundi hivyo wakikiri wazi kwamba mikopo hiyo imewasaidia kujikwamua kiuchumi. Vikundi vilivyotunukiwa vyeti ni pamoja na Kikundi cha Utulivu, Kikundi cha Wanawake katikati ya mji, Kikundi cha Umoja, Kikundi cha Star women na vingine.
Kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi afisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya ndugu Vincent Msolaa akimuwakilisha Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Tamimu Kambona amesema halmashauri ya wilaya ya Chunya Itaendelea kutoa mikopo kwa mujibu wa miongozo ya serikali kwa vikundi mbalimbali vya wanawake ili kuinua uchumi wao huku akisema zaidi ya shilingi milioni mia moja na arobaini (140) zimetolewa kwa vikundi vya wanawake wilayani Chunya
Msolla amewataka wanawake wilayani Chunya Kuchukua tahadhari ya vitendo vya Ushoga vinavyotokana na mmomonyoko wa maadili huku akiwakumbusha kuhakikisha wanawadhibiti watoto kutoangalia katika mitandao mbalimbali ya kijamii na televisheni mbalimbali mambo ambayo sio mweleko wa maadili yetu Tanzania.
Oliver Mtandi ambaye ni mkaguzi msaidizi Jeshi la Polisi wilayani Chunya amewata wanawake kuwa imara katika kuhakikisha maadili yanalindwa kwani Mama anayo nafasi kubwa sana katika malezi na makuzi ya Mtoto kwani mmonyoko wa maadili unaonekana sasa inasabibishwa na wanawake kutokusimamia vizuri nafasi zao. Kwa upande wa jeshi la polisi amesema wamejipanga kushirikiana na wananchi hivyo amewataka kutoa taarifa pale wanapoona uvunjifu wa amani unajitokeza
“mwanamke ni mjenzi wa kwanza wa familia yake, ndiye mlinzi wa kwanza wa familia yake, sisi wanawake tunaweza kujenga nyumba zetu na tunaweza kubomoa nyumba zetu kwani maandiko yamezungumza wazi. Jeshi la polisi tuko tayari kushirikiana na wananchi hivyo toeni taarifa pale unapoona ukatili unafanyika
Awali akisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kampeni ya kupinga ukatili inayojulikana kama Shujaa wa maendeleo na ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Bi Tunsume Kibweja amesema wilayani Chunya wanawake bado wanapambana na ukatili mkubwa katika maeneo mbalimbali ikiwepo ukatili wa kiuchumi
“Katika wilaya yetu wanwake wengi wanakosa fursa za kushirki katika biashara jambo linalosababisha baba peke yake kutegemewa kwa kila kitu, lakini wanawake wanayimwa haki ya kupata elimu na hata kumiliki maliza”
Bi Kibweja amesema pia maambukizi ya UKIMWI wilayani Chunya ni makubwa kwa wanawake ukilinganisha na wanaume na hii ni kutokana na wanawake kukosa nguvu ya kuamua ni muda gani hata kuingia katika mahusiano au kutokuingia katika mahusiano lakini pia maambukizi mengine husababishwa na ukatili wa kingono ambao unafanywa kwa wanawake
Diwani wa kata ya Matundasi ilyoko Mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya Mhe Kimo Choga amewashukuru watu wote waliohudhuria katika maadhimisho hayo huku akisema wanawake ni msingi wa maendeleo kwenye kata ya matundasi hivyo amewataka wanaume kuwaunga mkono wake zao katika kuhakikisha maendeleo katika ngazi ya familia, jamii na hatimaye TAIFA kwa ujumla
"Nawaomba wanaume wenzangu tuunge mkono jitihada za wake zetu (Wanawake) ili kuhakikisha tunapata maendeleo kwenye familia zetu na Mimi nitahakikisha nahimiza wanaume kuendelea kupinga ukatili kwa wanawake na ikiwezekana tuachane na Nyumba zetu za kando" amesema Mhe Choga
Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani katika wilaya ya Chunya yamefanyika katika kata ya Matundasi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni “Ubunifu na Mabadiliko ya kiteknolojia: Chachu katika kuleta usawa wa kijinsia” yamehudhuliwa na viongozi mbalimba wa serikali na taasisi binafsi ili kupaza sauti pamoja na Mwanamke ili hatimaye nia ya serikali ya awamu ya sita ya kumkomboa mwananchi wake katika Nyanja mbalimbali inatimia
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya Ndugu Vincent Msolla akizungumza mbele wa watu katika Madhimisho ya siku ya Mwanamke
Meza kuu wakifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitumbuiza
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.