baadhi ya viongozi na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Chunya wamejitokeza na kuzungumza mambo mbalimbali kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 8-8-2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (sapanjo).
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu ramadhan shumbi ameeleza kuwa kikao hicho ilikuwa kifanyike tarehe 30-7-2021 ila kutokana na changamoto mbalimbali kilisogezwa mbele na kufanyika tarehe leo 18-8-2021
Aidha kaimu mwenyekiti ameeleza kuwa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2020-2021 ilikuwa ni bilioni 5.2 lakini mpaka kufikia tarehe 30.06.2021 makusanyo yalikuwa ni bilioni 3.9 sawa na 75.3%
Baraza la maiwani pia liliishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuiwezesha Chunya katika miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja nakuleta fedha za maendeleo kiasi cha Tsh milioni 750 awamu ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2020/21 na kiasi cha Tsh milioni 720.6 kwa mwaka wa fedha 2021/22 na jingo kwa sasa lipo katika hatua ya upauaji.
Kwa upande mwinge Kaimu Mwenyekiti amewataka madiwani na Wataalamu kuendelea kuwa waadilifu,wakweli na wawazi wakati wanatimiza majukumu yao
Aidha kwenye swala la Afya, baraza hilo la Waheshimiwa Madiwani limehimiza wananchi kuwa na bima ya afya (Ichf iliyoboreshwa).
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ndugu Ramadhan ndiyo mwakibuka amesisitiza ukusanyaji wa mapato,kutangaza fursa za uwekezaji kupitia tovuti ya Halmashauri ,kujibu hoja zote za Wakaguzi (Ndani NA Nje),waajiriwa wapya kupata stahiki za kiutumishi kwa wakati.
Naye katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya nduguCharles Jokely Seleman amewapongeza madiwani waC.C.M kwa kutekeleza vizuri ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa mwaka 2020/2021.
Kuhusu utata wa zao la Tumbaku na kampuni ya ununuzi , Ndg Selamani aliwahakikishia waheshimiwa Madiwani kwamba amelichukuwa kama mwakilishi wa chama ngazi ya wilaya na atalifikisha kwa viongozi wake wa juu ili kuona namna ya kumaliza utata huoambao umekuwa ukijitkeza kila mwaka.
Ndg Selemani(Katibu C.CM Chunya) alimtaka mwakilishi wa Mbunge kumfikishia Mh. Mbunge changamoto hiyo ya wakulima na kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ili naye afikishe kwenye ngazi za juu.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.