Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya chunya limeketi jana katika kikao maalumu cha kupitia taarifa ya hesabu za mwisho za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uliohitimishwa juni 30 mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya fedha za serikali za mitaa ya mwaka 2019 sura ya 290.
Akiwasilisha taarifa za hesabu za mwisho za halmashauri Mweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Rajab Lingoni amesema kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 juni 2022, halmashauri ya wilaya ya chunya imeandaa hesabu zake kwa mujibu wa kanuni kubalifu za utayarishaji wa hesabu, memorandamu ya fedha za serikali za mitaa, sheria za manunuzi wa umma na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali.
Ameongeza kwa kusema sheria ya fedha za serikali za mitaa ya mwaka 2019 sura ya 290 imeelezea majukumu mahususi ya halmashauri ya wilaya ambayo yamejikita katika sehemu nne, moja ni ukusanyaji wa mapato kupitia kodi, leseni, ada na tozo mbalimbali
Aidha kuonyesha matokea ya fedha zilizokusanywa kama zimetumika vizuri kwa kutayarisha hesabu zilizo sahihi, sehemu ya tatu nikutoa huduma bora kwa wananchi na sehemu ya nne ni kuleta amani utulivu na utawala bora.
Mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri imeweza kupokea na kukusanya kiasi cha Bilioni 27.9 sawa na asilimia 98 ya makisio ya bilioni 28.5 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali, mapato ya ndani wamekusanya bilioni 5.2 sawa na asilimia 108 ya makisiyo yao,
Matumizi mengineyo halmashauri imeweza kupokea milioni 856.8 sawa na asilimia 58 ya makisio na ruzuku ya miradi ya maendeleo halmashauri imeweza kupokea jumla ya bilioni 9.4 sawa na asilimia 101 ya makisio.
Lingoni amesema kutoka kwenye makusanyo ya ndani halmashauri ya wilaya ya chunya imepeleka kiasi cha shilingi bilioni 1.6 katika miradi mbalimbali ya maeneleo ikiwa ni sawa na asilimia 40.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya chunya Mh. Bosco Mwanginde amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa kupokea na kupitisha taarifa za hesabu za mwisho za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ili ziwasilishwe katika Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa fedha za Serikali.
Aidha amewapongeza wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya chunya kwa kuweza kuandaa taarifa hizo za hesabu kwa umakini na ufanisi mkubwa
Sambamba na hayo Mh. Mwanginde amewapongeza madiwani na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya chunya kwa kuzeza kukusanya mapato kwa asilimia 108 na kuvuka lengo.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.