Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mhe. Ramadhan Shumbi ahimiza wananchi wa Wilaya ya Chunya kuhakikisha wanabuni na kuibua miradi ya maendeleo ambayo wanauwezo wa kuikamilisha kuibua na kukamilisha kwa kujitoa kwa dhati kwenye nguvu kazi na uchangiaji wa fedha.
Mhe. Shumbi ametoa wito huo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili ya mwaka 2024/2025 kilichoketi leo Januari 29, 2025 kujadili taarifa za kamati ya kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“ Ni muhimu wananchi kuanzisha na kuibua miradi ya maendeleo na kuikamilisha kwa kufuata vigezo vyote kulingana na mahitaji ya jamii husika, waheshimiwa Madiwani na wataalamu fuatilieni kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yenu” amesisitiza Mhe. Shumbi.
Aidha, Mhe. Shumbi amelieleza baraza kuwa, miradi mingi ya maendeleo ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji huku mingine imekamilika na mingine ikiendelea kutekelezwa, miradi inayoendelea kutekelezwa izingatie ubora ili iweze kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyopangwa.
Katika hatua nyingine, Mhe. Shumbi amesisitiza azma ya kuendelea kukusanya mapato katika vyanzo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inaendelea pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato kwenye vyanzo hivyo.
Vilevile, Mhe. Shumbi amewataka waheshimiwa Madiwani, wataalam kutoka Halmashauri kutosubiri viongozi kutoka nje waone mapungufu kwenye miradi inayotekelezwa wakati viongozi hao wapo.
Naye, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya Bi. Marietha Mlozi amesema Halmashauri imepanga kutoa mikopo Kwa vikundi themanini na tatu (83) kwa awamu ya kwanza kwav= vikundi vya wananwake, vijana na watu wenye ulemavu ambavyo vitakabidhiwa hundi ya Tsh. Milioni 803 siku ya Ijumaa, Januari 31, 2025.
“Vikundi 83 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vitakopeshwa mkopo wenye thamani ya Tsh. Milioni 803; kundi la wanawake watapata Tsh. Milioni 324, Vijana watapata Tsh. Milioni 468 na kundi la watu wenye ulemavu watapata Tsh. Milioni 11” amesema Bi Mlozi.
Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili cha kujadili na kupitisha taarifa mbalimbali za Kamati za kudumu za Halmashauri kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani, wataalamu mbalimbali wa Halmashauri, na Wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Wakili Athumani Bamba akisoma agenda za kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili ya mwaka 2024/2025 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mhe. Ramadhani Shumbi akiongeza baraza la Madiwani robo ya pili ya mwaka 2024/2025 liloketi leo, Januari 29, 2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri jengo jipya.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wakijadili kwa kina taarifa ya robo ya pili ya mwaka 2024/2025 ya kamati mbalimbali za kudumu kwenye ukumbi wa Halmashauri jengo jipya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.