Mkurugenzi wa kampuni ya tumbaku ya Amy Holdings, Ahmed Mansoor Huwel ambaye pia ni mnunuzi wa tumbaku kupitia kampuni yake tanzu ya Mkwawa Leaf ameahidi kuboresha maslahi ya wakulima wa zao hilo.
Huwel ameyasema hayo jana Wilayani Chunya wakati wa utambulisho wa kampuni yake ya Amy Holdings kwa wananchi wa kata ya Lupa, utambulisho uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh Juma Homera.
“Tumekuja hapa kwa nia njema hatujaja hapa kunyang’anya tumbaku ya mtu, kwa msiojua Philip ni rafiki yangu na tunajuana nae sana tumemsaidia Philip toka mwanzo alivyofungua kampuni ya Premium,” alisema Huwel.
Huwel aliongeza kwa kusema wao kama Amy Holdings wamekuja na sera tofauti na sera mpya kwani hawajaja Lupa kunyang’anya ama kuiba tumbaku wa mtu.
Vilevile Huwel aliongeza kwa kusema anaamini kuwa na ushindani ni afya, kwani kunapokuwa na ushindani kunakuwa na afya kwa wakulima wengi.
Aidha, alisema kuwa lengo la kuinunua kampuni hiyo ni kuwasaidia watanzania ili kuwanyanyua kiuchumi.
“Shida kubwa waliyopitia wakulima wa Tanzania ndio hasa iliyonisukuma mimi kuweza kununua hii kampuni ya TLTC ili niweze kuwasaidia na kuwakomboa wakulima wenzetu wa nyumbani.” Amesema Huwel
“Niwahakikishie wakulima wote wa Tanzania wakiwepo wa hapa Lupa nimekuja kuwasaidia sijaja kuwanyang’anya wala sijaja kuwaibia nia yetu ni njema sana.” Aliongeza Huwel.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Homera amesema wao kama mkoa wanahitaji kuwe na Ushindani, kusuwepo na mtu mmoja ambaye atatawala soko.
“Tukasema kwamba hebu tulete ushindani, tuwe na kampuni zaidi ya moja, tunashukuru Waziri wa Kilimo, tunanshukuru sana ametuletea kampuni mpya ya Amy Holdings ambayo inanunua Tabora na maeneo mengine.” Alisema Homera.
Pia homera amewataka wakulima kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wanunuzi wote, aliyopo kwa sasa Premium na mnunuzi mpya ambaye ni Amy Holdings
“Mimi hapa nimekuja kutambulisha makubaliano ni ya kwenu wenyewe mnataka mumuuzie, mnataka kufanya nini ni nyinyi wenyewe.” Alisema Homera
Vilevile amewaasa wakulima ambao tayari wameshaingia mikataba na Kampuni ya Premium kutovunja mikataba hiyo bali washirikiane nao kwani wamekuwa nao kwenye shida na raha.
“Kama kuna tumbaku imezidi na una uwezo wa kuuza kwa kampuni nyingine nenda kauze, maana mkataba si tani elfu nne na zipo tani elfu nne mia tano, mia tano hizo si gombania goli kila mmoja anaweza kuzichukua?
“Lakini msivunje mikataba mkalaza madeni mkamkimbia Premium mkaenda kwa kampuni nyingine, nendeni kwa step (hatua) kama mzigo upo wa kutosha unaweza kufanya option (chaguo) ya kwenda kwa mwingine lakini kama mzigo upo limit (idadi maalum) usihame kubalianeni na mkataba wenu malizaneni naye.
“Najua kwa changamoto hii huku kuna Premium huku kuna Amy Holdings bei lazima itachangamka sisi tutakuwa tunashangilia tu, nawajua Premium wananunua Mpanda, nimekaa nao hii Mbeya nimekaa nao na nipo nao lakini lazima tulete kampuni nyingi zaidi ili bei iwe nzuri kwa wananchi.” Alisema Homera
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Juma Homera akizungumza na Wananchi wa Kata ya Lupa wakati wa Kutambulisha Kampuni Mpaya ya Ununuzi wa Tumbaku wilayani Chunya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Amy Holdings Campany Limited Ndg. Ahmed Huwel Akiwa kwenye Mkutano wa kutambulishwa kwa kampuni yake ya Ununuzi wa Tumbaku kwa Wananchi wa Kata ya Lupa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.