Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya anawatangazia wananchi wote kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa Mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 155 [1] cha Sheria ya Serikali za Mitaa [Mamlaka za Wilaya] Sura 287 inakusudia kutunga Sheria Ndogo zifuatazo;
1.Sheria Ndogo za (Ada na Ushuru) za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
2.Sheria Ndogo ya (Kodi ya Huduma) ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
3.Sheria Ndogo za (Ushuru wa Maegesho) za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
4.Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii – Tiba Kwa Kadi) za Halmashauri za Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
5.Sheria Ndogo Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
6.Sheria Ndogo za Kudhibiti Afya na Usafi wa Mazingira za Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
7.Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Ardhi Mazingira na Uchimbaji wa Madini) za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
8.Sheria Ndogo za (Maendeleo na viwanda) za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
9.Sheria Ndogo za (Kudhibiti Mahudhurio ya Wanafunzi) za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya za Mwaka 2018.
Kwa hiyo, Wananchi wote mnatangaziwa kushiriki katika kutunga Sheria Ndogo hizo kwa kutoa maoni, hoja au pingamizi vile unavyoona inafaa.
kwa kusoma sheria hizo kiundani tafadhali bonyeza hapa RASIMU YA SHERIA NDOGONDOGO WILAYA YA CHUNYA.pdf
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.