UTANGULIZI:
Wilaya ya Chunya inafursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta za madini, kilimo, mazao ya misitu na nyuki, Utalii na Mali Asili, Pia bidhaa mbali mbali kutoka kwa wajasiriamali ambazo ni pamoja ni Asali ya nyuki wakubiwa na wadogo, mafuta ya Alizeti, bidhaa mbalimbali za mbao(Samani) , watu wote mnakaribishwa kuchangamkia fursa hizi za uwekezaji.
UCHIMBAJI WA MADINI:
Wilaya ya Chunya inautajiri mkubwa wa dhahabu na shughuli za uchimbaji na uwekezaji zilianza zamani kabla hata ya uhuru wa Tanganyika, wawekezaji wakubwa na wadogo wanaendelea na shughuli za uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya wilaya na hivyo kuchangia katika kutoa ajira na mapato kwa serikali na Halmashauri..
Yapo maeneo maalum yaliyotengwa kwaajili ya wachimbaji wakubwa, kati na wadogo hivyo wawekezaji wa ngazi zote mnakaribishwa kuja kuwekeza
KILIMO
Asilimia 87 ya wakazi wa wilaya ya Chunya wanategemea kilimo na kilimo ndiyo huchangia kwa kiwango kikubwa sana uchumi wa Wilaya
Wilaya inakadiriwa kuwa na jumla ya eneo lenye ukubwa wa hekta 1,315,000 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo linakadiriwa kuwa ni hekta 1,035,400 na jumla ya hekta 79,072 ndizo zilizotumika kwa kilimo cha mazao ya chakula, biashara na bustani (mboga na matunda)..
Wilaya ina wastani wa joto kati ya nyuzi za sentigredi 21 na 23. Wilaya hii hupata aina moja ya mvua (Unimodal rainfall pattern) yenye wastani kati ya milimita 500 na 1000 kwa mwaka. Msimu wa mvua huanzia mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi Aprili na kipindi chenye mvua nyingi ni kati ya mwezi Januari na Machi.. Yapo pia maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji hivyo wawekezaji wanakaribishwa sana.
.Mazao mbali mbali ya chakula na bishara yanastawi vizuri ndani ya wilaya ambayo ni pamoja na Mahindi, Maharage, Mtama, Karanga, Viazi vitamu, Ulezi, Mihogo, Alizeti, Tumbaku, Kunde, Choroko, Mihogo, Viazi vitamu na ulezi.
MALIASILI NA UTALII
Wilaya ya chunya ni moja kati ya maeneo yaliyosheheni Rasilimali maalum na muhimu kwa utalii . Maliasili zilizosheheni mtawanyiko wa mimea , Msitu na Wanyamapori mbalimbali zikiwemo sehemu zenye mambo ya kale, kihistoria, Chemichemi za maji moto na maumbile ya kuvutia ya Milima na miinuko yenye uoto wa asili.
FURSA ZA UTALII
Biashara ya uwindishaji kitalii inafanyika Chunya kama njia ya uvunaji endelevu wa wanyamapori, kuna uwepo wa wanyama pori karibia wote wa BIG 5 isipouwa kifaru, kuna TWIGA MWEUPE kama mnyama wa kipekee ktk ikolojia ya hifadhi ya majini ya Chunya-Rungwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
kuna uoto Pekee uliosheheni misitu ya miombo na mininga , milima ya kihistoria na matambiko mf. Ml. Mwene).
Chunya inapitiwa na barabara ya kihistoria ya kutoka kaskazini mwa Afrika mji wa Cairo hadi kusini mji wa Cape Town, Afrika kusini.(The Great North Road). Chunya imeunganishwa na barabara ya lami kwenda uwanja wa kisasa wa Songwe International Airport. .
UFUGAJI WA NYUKI
Wilaya ya Chunya ni mojawapo ya Wilaya zinazozalisha Asali na Nta kwa wingi Tanzania. Uoto wa asili wa miti aina ya Miombo ambayo ni malisho ya Nyuki na hali ya hewa inachangia sana katika shughuli za uzalishaji. Uwepo wa aina mbalimbali wa miti ya miombo inayochanua kwa misimu tofauti husaidia upatikanaji wa chakula cha nyuki kwa mwaka mzima. Wilaya ya Chunya inazalisha sana Asali ya Nyuki Wakubwa na Wadogo pamoja na Nta. Wastani wa uzalishaji wa asali kwa mwaka ni tani 408.54 na Nta ni tani 25.2. Kuna fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya Nyuki Wilayani Chunya kama Kuanzisha manzuki (Appiary), kuuza vifaa vya U nyuki kama vile Mizinga ya Kisasa, vifaa vya kuchakatia, mavazi ya kinga na Kuanzisha viwanda vya kuchakatia mazao ya nyuki.
Maeneo ya uwekezaji yaliyopo katika wilaya ya chunya ni saba (7) yenye jumla ya ekari 2758.86, Tunakaribisha wawekezaji wazawa na wa kigeni ili kuwekeza katika wilaya yetu. Maeneo hayo yapo kiwanja, itewe, makongolosi, kibaoni, mbugani, sinjilili, na lupa ambayo yanapatikana katika tarafa zote mbili za kiwanja na kipembawe
Fursa za uwekezaji zilizopo katika wilaya ya chunya ni kwenye viwanda na biashara. Viwanda vifuatavyo vinaweza kuwekezwa.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.