Ziara ya mhe. Waziri wilayani Chunya imelenga kukagua kituo cha madini mkoa wa Mbeya kinachojengwa wilayani humo ambayo itatumika kutoa elimu ya uchimbji, uchenjuaji n.k.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa waziri aliwahimiza wajenzi ambao ni SUMA JKT kuhakikisha wanamaliza kazi hiyo ya ujenzi ifikapo tarehe 15/01/2018.
Pia alizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo migogoro ya wachimbaji yashughulikiwe ngazi za chini na siyo yasubiri mpaka viongozi ngazi za juu waje, kuwepo na ukaguzi wa mara kwa mara ya uchimbaji wa madini, leseni za uchimbaji wa madini ziendelezwe na siyo mtu kuiliki tu na hazifanyii kazi, wachimbaji waache kuuza madini(dhahabu) mbichi kwa masonara, wachimbaji na wafanyabiashara wa madini wafuate taratibu na sharia . Lingine alilosisitiza Mhe. Waziri Kairuki ni kwamba serikali kupitia Tume ya madini inashughulikia upatikanaji wa soko la madini na Halmashauri zitenge maeneo kwa ajili ya ujenzi wa masoko ya madini.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.