Waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko amefanya ziara ya kukagua na kutembelea shughuli za ujimbaji madini ndani ya wilaya ya chunya
Dkt Biteko ametembelea migodi ya Imuma investment Company limited, Frank Mbwilo na mgodi wa Singa Duwila iliyopo kata ya Sangambi wilaya ya chunya, ambapo amewapongeza kwa ujimbaji wa kisasa wanaoufanya
"Nawapongeza kwa sababu mmejaribu kupiga hatua kufanya uchimbaji wa kisasa na kuongeza nguvu kuhama kwenye uchimbaji wa kubahatisha kwenda kwenye uchimbaji wa uhakika".
Dkt Biteko amewahakikishia kuwa serikali inatambua changamoto walizonazo wajimbaji na walisha tuma watu wa Tanesco kwenda kufanya tathimini ya mahitaji ilikuhakikisha wachimbaji wanapata umeme wa uhakika wa kuendesha miradi yao.
Aidha Biteko amewapongeza na kuwataka wachimbaji kuendelea kuchangia katika shughuli mbalimbali za kijamii.
"Imani yangu ni kwamba mteendelea kurudisha kwa jamii kidogo mnacho kipata ili jamii ijue hii miradi niya kwao" amesema Dkt Biteko
Kwaupande mwingine, Dkt Biteko amesema Serikali kupitia Taasisi ya Jiolojia Tanzania wanasogeza huduma za kimaabara katika mkoa wa kimadini chunya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji kupima sampuli za udongo na miamba.
Naye Mbunge wa jimbo la Lupa Mh. Masache Kasaka ameipongeza serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya kuhakikisha mazingira ya uchimbaji yanakuwa rafiki kwa wachimbaji wote na kuwawezesha kufanya shughuli zao vizuri zaidi
Pia amempongeza mheshimiwa waziri wa madini kwa kufanya ziara katika wilaya ya chunya na kutembelea miradi ya inayotekelezwa na wazawa.
Vilevile Masache amewataka wachimbaji kubadilika na kuacha uchimbaji wa holelaholea na wakubahatisha kwenda kwenye kuwekeza katika uchimbaji wa mgodi mdogo na kufikia katika hatua ya CIP kama ambavyo wengine wanfanya.
Picha mbalimbali wakati wa Ziara
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.