Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mbaraka Alhaji Batenga amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya na vitongoji vyake kuhakikisha wanatunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji vinavyopatikani katika maeneo yao
Batenga ameyasema hayo leo tarehe 27/02/2024 alipokuwa anazungumza na wananchi wa Matwiga wakati wa ziara yake yakukagua miradi mbalimbali kikiwepo chanzo cha maji cha Matwiga kwa lengo la kutambua namna ambavyo kitatoa huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kuwataka wananchi kutunza Mazingira
Wakati huo huo Batenga amemtaka meneja RUWASA Wilaya ya Chunya Mhandisi Leon Kavishe ndani ya Wiki moja kutembelea eneo la chanzo ili kuweka mazingira sawa ya utunzaji wa Mazingira ili kuufanya mradi huo unadumu kwa muda mrefu.
“Kama mnavyojua mradi huu sio wa jana kweli au si kweli mradi huu ni wa siku nyingi kwanini siku zote ulikuwa haujakamilika mpaka saizi ndio uweze kukamilika hiyo ni nia ya dhati ya Mh Rais kuhahakisha kwamba anatatua kero ya maji hasa vijijini”
Aidha Mhe Batenga amesema Kutokana na ukubwa wa mradi huo na uwingi wa maji yanayopatikana katika mradi huo inawezekana pia kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji ili kukuza shughuli za kilimo cha umwagiliaji wa maeneo hayo na hatimaye kuongeza uchumia wa mwananchi mmoja mmjoa na hata Taifa kwa Ujumla
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mhe Frank E. Malambughi amemuomba mkuu wa Wilaya kukitazama chombo kilichowekwa kusimamia uendeshaji wa huduma hiyo akidai haujitoshelezi ukilinganisha na ukubwa wa mradi
Hata hivyo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Chunya amesema kuwa mradi huo umetumia zaidi ya Bilioni mbili ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa kusafirishia maji,Jengo la mitambo na huduma nyingine nyingi
Tarura nao hawakubaki nyuma katika kutoa majibu sahihi juu ya hatua waliofikia ya ujenzi wa barabara inayofika katika eneo hilo la mradi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja katika eneo hilo ambapo amesema kuwa mradi huo utawekwa kwenye mpango mwaka wa fedha ujao kwani mwaka huu haujaingia katika mpango huo
Ziara ya Mkuu wa wilaya ya inataraji kudumu kwa siku mbili ambapo leo ikiwa ni siku ya kwanza ametembelea miradi mbalimbali ikiwepo mradi wa Maji, ujenzi wa Shule ya Msingi Tulieni, kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu
Kaimu Meneja RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Leon Kavishe akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Chunya aliambata na kamati ya Ulinzi na usalama kukagua miradi Mbalimbali inayotekelezwa wilayani Chunya
Baadhi ya Mitambo iliyofungwa katika mradi wa maji Matwiga
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Batenga (Aliyetangulia Mbela) akiongoza Msafara wa kamati ya usalama wilaya ya Chunya kukagua miradi ya Maendeleo (Pichani wakikagua mradi wa Maji Matwiga)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.