Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Mkala amefanya ziara katika Kata ya Matundasi Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambapo
amekagua maendeleo ya ujenzi wa makazi ya muda mfupi(Camp) kwa wajenzi wa Barababra ya Chunya - Makongolosi kwa
kiwango cha Lami. Akiwa hapo alipokea taarifa fupi ya mradi huo.
Mkuu wa Mkoa akipata maelezo ya Mradi huku Mkuu wa Wilaya Mh. Rehema Madusa na Diwani wa Kata ya Matundasi wakisikiliza kwa makini.
Kampuni inayohusika na ujenzi huo Imeelezea baadhi ya Changamoto wanazokutana nazo kuwa ni maji na wizi ambapo katika uwasilishaji wa taarifa yao wamesema wameanza kuibiwa baadhi ya vitu zikiwemo nyaya za umeme..
Mkuu wa Mkoa katika kikao chake na wananchi aliwaombaa kuacha tabia mbaya za wizi kwani amewahakikishia kupewa kipaumbele kwenye ajira katika Mradi huo. Kuhusu changamoto ya maji kampuni husika inachimba kisima kirefu kukabiliana na changamoto hiyo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mkuu wa Mkoa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.