Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya chunya Bi. Sophia Kumbuli anapenda kuwakaribisha wananchi wote wa wilaya ya Chunya kuhudhuria katika ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli ambaye ameingia mkoani mbeya tar 25/04/2019.
Pamoja na mambo mengine tarehe 27/04/2019 Mheshimiwa Rais atafika wilayani Chunya kwaajili ya matukio yafuatayo;
1. Uzinduzi wa barabara ya Mbeya - Chunya pamoja na kusalimia wananchi wa Chunya mjini katika eneo la uwanja wa sabasaba Chunya mjini.
2.Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Chunya - Makongolosi.
Wananchi wote mnakaribishwa kumlaki Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli katika ziara hiyo.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.