Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamis Kigwangala akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Chunya ambapo aliwasili
Makao Makuu ya wilaya na kupokewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Rehema Madusa, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya,
viongozi wa Chama Tawala, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri, pamoja na wakuu wa idara mbalimbali za
serikali kuu na Halmashauri. Punde baada ya kuwasili Mkuu wa wilaya ya Chunya alimkaribisha na kisha kumsomea taarifa fupi
ya wilaya ambapo kubwa zaidi aligusia juu uvamizi wa wanachi katika maeneo ya hifadhi na kugusia kuwa operesheni zilianza
tangu zamani akitolea mfano mwaka 2013 na 2015 zilifanyika operesheni za kuwaondoa wavamizi hao, lakini maeneo hayo bado
yanaendelea kuvamiwa akitolea mfano msitu wa hifadhi wa TFS wa kipembawe wenye hekta takribani 6000.Pia juhudi zimeendelea
kufanyika na Serikali ya Wilaya ya sasa kwani nayo imeendesha Operesheni ya kuwaondoa wavamizi na kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa. akigusia pia vitalu viwili chini ya wilaya vya Piti East na Chunya west amabavyo navyo vimevamiwa, Pia
aliendelea kusema kuwa wakati wa operesheni za kuawaondoa wavamizi mali nyingi ziliweza kukamatwa ikiwemo na magogo
yaliyokutwa ndani ya msitu wa hifadhi kinyume cha sheria na taratibu.
alipopewa nafasi ya kuongea Mhe. Waziri alianza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla kwa kumpokea vizuri
tangu alipoingia katika mkoa wake na kusema lengo la ziara hii ni kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali
za Maliasili, akaendela kuleza kuwa Maliasili ni za nchi nasiyo za wizara ya Maliasili na wao kama wizara ni waangalizi tuu.
aliendelea kueleza kuwa Serikali ya wilaya inamamlaka ya kusimamia utekelezaji wa sheria katika eneo husika. akigusia
suala la uhifadhi wa msitu wa Patamela Mhe. waziri alisema wao kama wizara wamepewa msitu bila kujali umepitia kwenye
wilaya gani na akamshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kuweza kushughulikia mgogoro uliojitokeza na kuumaliza. aliendelea
kugusia kuwa majangili wanaishi na wananchi hususani kwenye vijiji vinavyozunguka mapori ya akiba hivyo kuiomba serikali ya wilaya kuongeza juhudi.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alipata pia fursa ya kukagua uvamizi uliofanyika katika Msitu wa hifadhi wa serikali kuu wa
Itengu kata ya kibaoni, ambapo aliweza kubaini uharibifu wa mazingira, uchimbaji wa madini kinyume na taratibu pamoja
makazi yalijengwa kiholela.
Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya mwaoga ambapo Mhe. Waziri alianza kwa kusikiliza
kero za wananchi ambazo nyingi ya kero zilikuwa ni juu wawekezaji kujitwalia maeneo makubwa na wananchi kukosa sehemu za
uchimbaji, pamoja na mkanganyiko unaotokea wananchi wanapokamatwa ndani ya msitu wa hifadhi na kwenda kufunguliwa mashtaka
wilaya jirani ya Songwe. kero ambazo hazikuwa chini ya wizara ya Maliasili moja kwa moja na kumpa nafasi Mhe. Mkuu wa Mkoa
kuzitolea maelezo, Mbali na kujizotela maelezo kero hizo aliahidi kuwa atamleta waziri wa Madini ili nae aje atoe majibu na
dukuduku la wananchi.
Akiwahutubia wananchi katika kata ya Mwaoga Mhe. Waziri alianza kwa kusema jukumu alilopewa la uwaziri ni gumu na kamwe
hakulifurahia pindi alipoteuliwa bali alimshukuru Mungu kwani Maliasili ni uhai wa nchi, na kutokana na utunzaji wa
maliasili unapata maji, chakula, umeme n.k. aliendelea kusisitiza na ninanukuu "Misitu ya hifadhi ni hifadhi, Wizara ya
Maliasili inatetea Misitu na Wanyamapori na ukikamatwa ndani ya hifadhi utachukuliwa hatua kali kama jangili mwingine tu"
mwisho wa kunukuu. Pia Mhe. waziri alimpa nafasi Mkurugenzi wa Huduma za Misitu (TFS) ili atoe taratibu za wananchi
kuchimba ndani ya hifadhi ambaye alisistiza kuwa ili uweze kuchimba ndani ya hifadhi mwananchi ahakikishe anapata leseni
kutoka wizara ya Madini, na kwamba lazima kwanza tathmini ya uharibifu wa mazingira ifanyike ili kubaini athari na
kutafuta njia ya kudhibiti. aliongeza ukikutwa unachimba bila vibali mali zako zitataifishwa na kufikishwa kwenye vyombo
vya Dola.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.