Katika ziara hiyo Mh.Mkuu wa Wilaya aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya chunya Bi. Sophia Kumbuli, Kamati yake ya ulinzi na Usalama, , Afisa madini (W)Mhandisi (W) pamoja na Afisa Elimu Sekondari (W).
Lengo hasa la ziara ya Mheshimiwa mkuu wa Wilaya ni:
1. Kufanya kikao kifupi na uongozi wa Sunshine Mining juu ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Matundasi
2. Kufika katika shule ya sekondari Matundasi kuona ilipofikia katika ujenzi wa maabara,madarasa na nyumba ya walimu.
3. Kufanya kikao na wananchi wa Kata ya Matundasi
Mh.Mkuu wa wilaya alianza kwa kuonana na uongozi wa mgodi wa Sunshine ambao ndio wanaojenga maabara katika shule hiyo ya Matundasi kama sehemu ya kurejesha sehemu ya faida kwa jamii. Katika kikao kifupi cha ndani na uongozi wa Sunshine mining, Mh.Madusa aliomba uongozi wa mgodi huo kufanya haraka kukamilisha ujenzi wa maabara mbili ambazo wameshapauwa na aliwaambia ni vizuri ikiwa tayari ndani ya miezi miwili kuanzia leo tarehe 11/01/2018 pamoja na changamoto mbalimbali walizoeleza. Uongozi wa Sunshine Mining waliahidi kufanya kama ilivyoombwa na Mh.Mkuu wa wilaya.
Mh. Rehema Madusa (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Sophia Kumbuli (Wa kwanza kushoto) wakiwa ndani ya moja ya maabara katika shule ya Sekondari Matundasi pamoja na uongozi wa Sunshine Mining.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alimalizia ziara yake kwa kufanya Mkutano na wanachi wa Kata ya Matundasi .Katika Mkutano huo Mheshimiwa Diwani(Kimo J.Choga) alimpongeza Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi mtendaji kwa uchapaji kazi wao mzuri, Pia Mh.Diwani alisema wana miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inaendelea, iliyokamilika na mengine ipo kwenye mipango ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Zahati Itumbi ambayo Sunshine wataijenga na kupauwa lakini umaliziaji mwingine utafanywa na wananchi.
Mkuu wa Wilaya akizungumza na wanachi.
Mh.Rehema Madusa(mwenye miwani), Mkurugenzi Mtendaji kushoto kwake Bi. Sophia Kumbuli wakisikiliza kero za wananchi.
Kulia kwa Mkuu wa wilaya ni Mh.Diwani kata ya Matundasi na Mwenyekiti wa mtaa “A”
Mkurugenzi Mtendaji alipata pia nafasi ya kuongea na wananchi ambapo aliwaeleza vigezo vya shule kusajiliwa na kuruhusiwa kuchukua wanafunzi . Vigezo hivyo ni
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya
Ulipofikia ujenzi Jengo la Utawala Shule ya sekondari Matundasi
Ulipofikia Ujenzi wa Majengo ya Maabara katika Shule ya Sekondari Matundasi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.