Mkuu wa wiaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga ameiongoza Kamati ya Usalama wilaya kwenye ziara ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza kufanyika kwa Mafunzo Elekezi kuhusu Mfumo wa manunuzi serikalini NeST kwa Mafundi wazawa pamoja na wafanyabiashara wanaopatikana kwenye maeneo inakotekelezwa miradi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi ya Serikali katika maeneo yao
Ametoa kauli hiyo wakati wa akihitimisha ukaguzi wa miradi dakika chache baada ya kukagua ujenzi wa Mabweni ya wasichana na wavulana katika Shule ya Sekondari Sangambi ambapo amesema moja ya Changamoto inayochelewesha miradi yetu ni kutumia mafundi wanaotoka nje ya eneo ambapo mradi unatekelezwa
“Ujio wa Mfumo wa NeST umefanya Mafundi wale wale tuliokuwa tunawatumia awali kabla ya mfumo leo kubaki kama Wapenzi watazamaji na sababu ni kutokuwepo kwenye Mfumo hivyo nimetoa maagizo Mafundi wote wapewe Mafunzo na wasaidiwe kujisajili kwenye mfumo huo ili waweze kuomba na kutekeleza kazi Mbalimbali za ujenzi wa Miradi ya Serikali kwenye maeneo yao wanayoishi” Amesema Mhe Batenga
Aidha Mhe Batenga amesema kwasasa Chunya ni tulivu na salama huku akiwapongeza wananchunya kushiriki kwenye zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambalo limepita salama na tayari viongozi wamepewa majukumu yao na wameoneshwa miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao tayari kusimamia miradi hiyo
Pia Mhe. Batenga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kutoa Fedha nyingi wilaya ya Chunya ambapo kwa ziara hii tu miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni moja na milioni mia nne imekaguliwa na hiyo inshara kwamba tuna miradi mingi sana inatekelezwa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Cuthberth Mwinuka amesema Maelekezo ya Mkuu wa wilaya ya Chunya yamepokelewa na yatatekelezwa kuanzia tarehe 17/12/2024 kwa kuanza kutoa mafunzo na maelekezo kwa Mafundi wazawa juu ya mfumo wa manunuzi pamoja na wafanya biashara ili kurahisisha utekelezaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Kamati ya usalama wilaya ya Chunya imehitimisha ziara yake ya siku mbili iliyoanza tarehe 10/12/2024 na imehitimishwa tarehe 11/12/2024 na miradi yenye thamani ya Zaidi ya milioni moja na milioni mia nne imekaguliwa pamoja na kuonya, kuhimiza na kuhakikisha usimimizi unaongezeka ili miradi iwe bora na yenye kuakisi kiasi cha fedha zilizotolewa na Serikali
Ujenzi wa Daharia ya Wasichana Shule ya Sekondari Isenyela ni moja kati ya Miradi ilitotembelea na kamati ya usalama wilaya ya Chunya na imekuta mradi unaendelea kutekelezwa huku kamati ikishauri nguvu na ushirikishwaji wa wadau wa maendeleo kuongezeka sana
Kamati ya Usalama ikikagua ujenzi wa Miundombinu ya Bweni la wanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Makongolosi Chunya inayotaraji kupokea wanafunzi Mwezi Julai 2025
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.