Watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wamepewa elimu ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto ambayo yanaweza kutokea na kusababisha upotevu na uharibifu wa mali wakati mwingine kusababisha hata vifo pindi janga la moto linapotokea na kushindwa kudhibitiwa kwa haraka
Elimu ya kukabiliana na majanga ya moto imetolewa vitendo na kampuni ya Saragana interprises huku ikienda sambamba na kufunga vizimamoto (fire extinguisher) katika maeneo mbalimbali ya jengo la Utawala
Fundi kutoka kampuni ya Saragana ndugu Salehe Daniel ametoa mafunzo kwa watumihi juu ya namana ya kutumia kizima moto (fire extinguisher) pindi janga la moto linapotokea na kuweza kukabiliana nao ili usiweze kuleta majanga makubwa Zaidi
Salehe amesema kuwa lengo kubwa la kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto katika taasisi mbalimbali ni kuwawezesha wananchi kujua namna ya kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto yanapotokea.
“Wananchi wengi hawana elimu ya namna ya kujikinga nakukabiliana na majanga ya moto hivyo kampuni yetu imekuwa ikitoa elimu ya jinsi kuzia majanga ya moto yasitokee lakini pia njinsi ya kukabiliana na janga la moto pindi linapotokea ili lisiweze kusababisha madhara makubwa Zaidi". Alisema Salehe.
Aidha Salehe amewaasa watumishi kuhakikisha wanakuwa na kizima moto (fire extinguisher) majumbani mwao lakini pia kwenye magari ili kuweza kukabiliana na janga la moto linapotokea wakati wanaposubiri Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika eleo la tukioa hali inayoweza kuzuia au kupunguza uharibifu ambao ungeweza kutokea
Pius Ambros, Salma Nyangwa na Enock Mbala wakiwawakilisha watumishi wengine katika zoezi la kuzima moto wamemshukuru Mkurugenzi Mtendaji ndugu Tamim Kambona kwa kuleta kampini ya Saragani enterprises kuja kuwapa elimu ya jinsi ya kupambana na majanga ya moto ambapo wameweza kujifunza namna ya kutumia kizimamoto na jinsi ya kuzima moto kwa vitendo unapokuwa umetokea.
Salehe Dabniel Fundi kutokakampuni ya Saragana Interprises akiwasha moto kwaajili ya kuwawezesha watumishi kuzima kwa vitendo kwa kutumia kizima moto ( fire extinguisher) kama ambavyo wamepewa elimu hiyo
ya jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto
Ndugu Salehe Daniel Kutoka kampuni ya Saragana Interprises akimwelekeza bi Salma Nyangwa kwa niaba ya watumishi wengine waliokuwepo namna ya kuzima moto kwa kutumia kizima moto ( fire extinguisher) baada ya kupata mafunzo ya jinsi ya kutumia kizima moto hicho.
Ndugu Enock Mbala miongoni mwa watumishi waliopewa mafunzo ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto akizima moto baada ya kupatiwa mafunzo ya namna ya kuzima moto kwa kutumia kizima moto ili kuhakikisha moto wote unazimika kabisa na kuacha mazingira katika hali ya usalama.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.