Waziri wa Madin wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anthony P. Mavunde ametoa onyo kwa baadhi ya watu wasio waaminifu wanaotorosha madin kuacha maramoja tabia hiyo kwani inachangia upotevu wa mapato katika nchi na kukwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu ,afya barabara, maji na mingine.
Ametoa onyo hilo leo tarehe 28/10/2023 kwa nyakati tofauti alipotembelea Soko la kuu la Madini la Halmashauri ya wilaya ya Chunya na Kituo cha Madini Itumbi wakati alipofanya ziara ya kutembelea Mkoa wa kimadini Chunya mapema leo.
“Nitumie fursa kuwataka watanzania wote hasa wale ambao wanaendelea kuijaribu serikali kuacha mara moja biashara hiyo ya utoroshaji wa madini kwani tutachukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kusimamisha na kufuta leseni ya biashara ya madini nchi nzima kwa mtu atakayebainika kufanya utoroshaji wa madini lakini pia kufwatilia mnyororo mzima wa watu hao kuanzia chini mbaka juu” alisema Mhe. Mavunde.
Awali akitoa salamu za wananchi wa wilaya ya Chunya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S.Mayeka ameipongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri katika sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na masoko ya dhahabu kwani masoko hayo yamesaidia kudhibiti mapato yatokanayo na uchimbaji wa Dhahabu suala linalopelekea Halmashauri kuendelea kuongezekana katika suala la ukusanyaji wa mapato.
Akitoa taarifa ya madini mkoa wa kimadini Chunya Afisa madini mkazi ndugu Sabahi Nyasiri amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na utoroshwaji wa madini unaofanywa na baadhi ya wachimbaji wasio waaminifu ambapo hivi karibuni wamefanikiwa kukamata dhahabu kg 6.9 kwa kushirikiana na kikosi kazi pamoja na jeshi la polisi.
“Tumeendelea kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa dhahabu pamoja na jeshi la polisi ili kuhakikisha tunawakamata watorashaji wa madini na hivi karibuni tumefanikiwa kukamata dhahabu ya kg 6.9 na hii ilikuwa ni kiu yetu ili kuhakikisha tnamsababishia mtu hasara kutokana utoroshaji wa madini"
Ziara ya waziri wa Madini imekuja ikiwa ni siku chache wilaya ya Chunya Imedhibiti utoshaji wa Madini ambapo imekamata madini kilogramu 6.9 zenye thamani ya zaidi ya zaidi ya shilingi milioni 961,000,000/= ambapo halmashauri ingepoteza zaidi ya Shilingi milioni sitini na nane (68,000,000/=)
Waziri wa Madini Mhe Mavunde akisalimia na viongozi mbalimbali wakati alipokuwa anawasili wilayani Chunya Waziri wa Madini Mhe Mavunde akionesha sehemu ya madini yaliyokamatwa yakitoroshwa kutokana wilayani Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.