WATENDAJI wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wamepatiwa mafunzo na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia mradi wa PS3+ uliofadhiliwa na watu wa Marekani.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watendaji hao katika nyanja za tenkolojia ya mawasiliano (TEHAMA), usimamizi wa rasilimali, utawala bora pamoja na ushirikishwaji wa wananchi.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, David Olelaput ambaye ni mratibu wa PS3+ Nyanda za juu Kusini alisema, mradi wa PS3+ umelenga kusaidia katika maeneo hayo ili kuleta tija katika jamii.
"Kwa kifupi leo hii tupo hapa kusapoti kwenye eneo la ushirikishwaji wa wananchi na utawala bora." Alisema Olelaput.
Naye Mataalam wa kamati ya Mkoa Mamlaka ya Serikali za Mitaa Bw. Nazar Sola amesema, mradi wa PS3+ unashirikiana na Serikali kuimarisha Mfumo wa Utawala bora kwenye Halmashauri.
"Lakini baada ya kufanya kazi hii kwa miaka kadha tumeona mambo hayatendeki kama tulivyotarajia, tumekuwa na majadiliano na TAMISEMI kwamba ni kwanini masuala ya Utawala bora hasa masuala ya ushirikishwaji wa wananchi hayafanyiki, mbao za matangazo na masanduku ya maoni hayafanyi kazi, mkutano watu hawahudhurii na bado taarifa toka kwenye vijiji zinaandikwa na kupelekwa Halmashauri.
"Wewe kama Mkurugenzi wa kata kazi yako ni kuratibu shughuli zinazofanyika kwenye kata yako, lengo la haya mafunzo ni kukumbushana juu ya uimarishaji wa mifumo ya utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi." Alisema Sola.
Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bw. Alex Batwel amewataka watendaji wa kata kuhakikisha yale yote waliyojifunza kwa siku mbili wanakwenda kuyafanyia kazi na kuleta tija na manufaa kwenye maeneo yao ya kazi na Halmashauri kwa ujulma.
"Utawala bora ni mpana sana, mmejifunza namna ya kuzingatia ufuataji wa taratibu na sheria zinazowaongoza kwenye ngazi zenu za kata, pia mmejifunza juu ya majukumu yenu, mipaka yenu na mahusiano kwenye taasisi zinazopatikana kwenye kata zenu.
“Nina imani haya mafunzo mliyoyapata yataenda kuboresha kile mlichokuwa mnakifanya aidha kwa mazoea au kwa kufuata utaratibu, mkaenda kufanya kikawa kizuri zaidi.” Alisema Batwel.
"Mkawasimamie watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji kuhakikisha wanasoma taarifa za mapato na matumizi, waitishe mikutano mikuu kwa mujibu wa sheria.
“Mkienda kusimamia hayo ndio mwisho wa siku tunasema utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi unazingatiwa." Alisisitiza Batwel.
Katika mafunzo hayo watendaji wa kata wamejengewa uwezo dhidi ya utawala bora ikilenga namna ya uendeshaji wa vikao, uandishi wa muhtasari wa vikao, ushirikishwaji wa wananchi katika kuandaa bajeti, kusomewa mapato na matumizi, matumizi ya mbao za matangazo pamoja na tovuti ya halmashauri ikiwa ni jukwaa la kutolea taarifa za maendeleo katika maeneo yao.
Mtaalamu wa Kamati ya Mkoa Mamlaka ya Serikali za Mitaa Bw. Nazar Sola akifafanua malengo ya Mradi wa PS3+ kwa washiriki walio Udhuria Mafunzo ya Utawala bora na Usimamizi wa Rasilimali
Mratibu wa PS3+ Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg. Simon Mbella akiwasilisha mada ya Utawala bora na Ushirikishwaji wa wananchi kwa Watendaji wa kata
Watendaji wa kata Wakiwa kwenye Mafunzo ya Utawala Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi yaliyo tolewa na PS3+ kwa kushirikiana na Serikali katika Ukumbi wa mikutano wa halmashauri
Afisa Tehama Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg Happygod Mollel akiwasilisha mada inayohusu Tovuti ya Halmashauri kwa Washiriki wa Mafunzo ya PS3+ katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Afisa Mipango Wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg Nerbart Gavu akiwasilisha mada ya O & OD iliyoboreshwa kwa Watendaji wa kata walioshiriki mafunzo ya Utawala bora yaliyotolewa na PS3+ kwa kushirikiana na Serikali
Watendaji wa kata wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo wakijifunza Mfumo wa MUKI
Mtaalamu wa Kamati ya Mkoa Mamlaka ya Serikali za Mitaa Bw. Nazar Sola akimwelekeza Mtendaji wa kata ya Makongolosi jinsi ya Kutumia Mfumo wa MUKI
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.