Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya manispaa ya Ilemela kwaajili ya kuongeza ujuzi na mbinu katika ukusanyaji wa mapato ikiwa ni jitihada za kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kukusanya mapato ya Halmashauri kwenye vyanzo mbalimbali vya Mapato.
Ziara hiyo ni kutokana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu kambona kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na watendaji wa kata katika ukusanyaji wa mapato zimepelekea Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato katika mkoa wa Mbeya hivyo ameamua kuwapa motisha watendaji hao ili kujifunza njia mbalimbali za ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya manispaa ya ilemela Mkoani Mwanza
Awali akielezea lengo la ziara hiyo Mkuu wa Msafara Afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Moses Ngole amesema kuwa ziara ya watendaji kata imelenga kujifunza namna mbalimbali za ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali ili sisi pia tukaendelee kuimarisha zoezi la ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Afisa Biashara wa Halmashauri hiyo Bi Elizabeth Swagi amefurarahishwa na ugeni wa watendaji kutoka Chunya na kusema kuwa kuna vitu ambavyo watajifunza kutoka kwao ikiwa ni pamoja na njia mbalimbali zinazotumika kukusanya mapato zinazoongozwa na sheria ndogo ndogo za Halmashauri.
Miongoni mwa njia za ukusanyaji wa mapoto walizojifunza watendaji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya ni pamoja na kutumia Mahakama inayotembea (Mobile court) ambapo njia hiyo imekuwa ikitumiwa na maafisa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pale ambapo wahusika wanashindwa kilipa mapato kwa utaratibu uliowekwa hivyo kufikishwa katika hatua za mahakama.
Nae Afisa mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ndugu Nicolaus Kawana ameeleza vyanzo mbalimbali vya mapato na jinsi ambavyo wamekuwa wakikusanya mapato katika vyonzo hivyo ikiwa ni pamoja na stendi ya mabasi, leseni za biashara , nyumba za kulala wageni na vyanzo vingine vingi ambavyo vimekuwa vikiingizia halmashauri hiyo mapato.
Wakiwawakilisha watendaji kata wenzao kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Ayubu Masota, , Egitho Bilali, Monica Magasha wameweza kuuliza maswali mbalimbali kwaajili ya kuongeza uelewa zaidi ikiwa ni pamoja na njia wanazotumia kukusanya ushuru wa taka, ushuru wa mabasi na nyumba za kulala wageni na ni kwa namna gani njia ya Mahakama inayotembe imefanikiwa na changamoto zake.
Ziara ya watendaji wa kata imejumuisha Maafisa Utumishi, Afisa biashara, Afisa Tehama, Afisa mipango na Uratibu na Mhasibu, ziara hiyo imedumu kwa siku moja na wameweza kutembelea baadhi ya vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na Stendi kuu ya mabasi ya Nyamhongolo na Soko la samaki Mwaloni ambapo wamejifunza na kujionea vyanzo mbalimbali jinsi vinavyoiingizia mapato manispaa ya Ilemela
Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wakijiandaa kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela tayari kwa Mafunzo
Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na maafisa wengine kutoka Makao makuu ya wilaya wakipewa maelekezo na Bwana Wilhadius Buberwa Meneja Uvuvi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.