Watendaji wa kata, vijiji na maafisa Ugani kutoka tarafa ya kipembawe wilayani Chunya wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili kuanzia jana tarehe September 27, 2023 kwa kata za Lupa, Upendo, Mamba, Lualaje, Nkung’ungu, Matwiga, Mtanila, na leo tarehe 28/09 28, 2023 mafunzo yameendelea kwa kata zaMafyeko na Kambikatoto.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo AfisaMipango wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Nebert Gavu amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu ngazi ya kata ili kuhakikisha wanaenda kuwaelimisha wananchi juu ya mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa.
“Tukitoka hapa tunatarajia kila kijiji kitakuwa na wawezeshaji jamii na mipango tutaipata kwa wakati, tunatarajia baada ya hapa mnaenda kuanza uwezeshaji kwenye vitongoji kule chini ili wananchi waweze kuuelewa huo Mfumo” alisema ndugu Nebert Gavu.
Gavu aliongeza kusema kuwa mafunzo haya yatawawezesha wataalamu wa ngazi ya kata kuwana ufahamu wa kina juu ya hali ya maendeleo katika maeneo yao na kuwa na uwezo wa kubuni mikakati inayowza kuleta maendeleo mtu mmoja mmoja na baadaye jamii na Taifa kwa ujumla.
Katika Mafunzo hayo wataalamu hao wamesisitizwa kushirikisha jamii katika kila hatua ya maendeleo ikiwa uibuaji na utekelezaji wa vipaumbele vya jitihada za jamii
Mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa unamtaka mwananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kupanga mipango kulingana na mahitaji halisi, uwezo wa kitaasisi, na rasilimali walizonazo, aidha uibuaji wa miradi ya vipaumbele, kuweka jitihada zao kwenye miradi hiyo.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na wawezeshaji Tisa, Ndugu Nebert Gavu, Bi Adeline Cosmas, Ndugu Nicholous Chambala, Ndugu Mjanaheri Swalehe, Ndugu David Ngowo, Ndugu Paul Lugodisha, Ndugu Pius Ambros, ndugu Fredy Mwangalaba, ndugu Christian Silomba wote kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya na Mafunzo hayo yanataraji kuendelea kwa wataalamu kutoka Tarafa ya Kiwanja
Afisa mipango Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Nebart Gavu akiendelea kutoa maelekezo kwa washiriki katika semina ya wataalamu Ngazi ya kata na vijiji katika Tarafa ya Kipembawe
Bi Adelin Cosmas (Mwenye fulana Nyekundu) akiongozo mjadala wakati wa mafunzo kwa wataalamu wa vijiji na kata wakati wa mafunzo katika tarafa ya kipembawe
Washiriki wa Mafunzo wakiendelea kufuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa wawezeshaji wakati wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Kipembawe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.