Wauguzi na wakunga hospitali ya wilaya ya Chunya wameadhimisha siku yao kwa kuwapatia wagonjwa zawadi mbalimbali.
Maadhimisho ya siku ya Wauguzi na wakunga duniani hufanyika kila inapofika Mei 12 kila mwaka ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa, “Wauguzi ni sauti inayo ongoza, wekeza kwenye uuguzi na heshimu haki na kulinda afya kwa wote."
Akizungumza wakati wa kuwapatia zawadi wagonjwa, Afisa Muuguzi katika hospitali ya wilaya, Dkt. Osman Simbeye amesema, wanayo furaha kuadhimisha siku hii na kumkumbuka mwanzilishi wa siku ya wauguzi duniani Mama Florence Nightingale.
“Ni siku yetu ya furaha kwa kuhudumia wagonjwa ndio maana mnaona tunapita kwenye wodi humu kuwaona na kuwapa zawadi." Alisema Simbeye.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaasa wauguzi wote kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagongwa wote wanaokuja kupata huduma katika hospitali hiyo ya wilaya.
“Niwaombe sana wauguzi wenzangu tuhakikishe tunatoa huduma bora na stahiki kwa kila mgongwa anayefika hapa hospitalini,” alisema simbeye.
Naye Kaimu Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dkt. Issa Mbande amesema, wao kama Halmashauri wameamua kufanya maadhimisho hayo kwa kuwapatia zawadi wagonjwa waliopo wodini.
"Tumefanya hivi kwa ajili ya kuonesha upendo kwa wagonjwa wetu na kumuenzi Mama Florence Nightingale mwanzilishi wa siku hii muhimu kwa wauguzi.
“Sisi kawa Wauguzi tunayo furaha kuadhimisha siku hii muhimu na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu." Alisema Dkt. Mbande
|
|
Wauguzi wa hospitali ya wilaya ya chunya wakiwa katika picha ya pamoja siku ya maadhimisho ya siku ya wauguzi yaliyofanyika katika hospitali ya wilaya
Katibu wa Afya halmashauri ya wilaya ya chunya Bi Chrispina Kasikiwe akimpatia zawadi moja ya mgonjwa wodini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.