Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga amesema kuwa Wananchi wana matumaini makubwa sana na Wenyeviti wa vijiji,Vitongoji na Wajumbe wa serikali za vijiji ambao wamewachagua wao wenyewe kwa kuwapigia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27/2024.
Kauli hiyo ameitoa leo Disemba 9/2024 wakati wa Mafunzo kwa wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa serikali za vijiji yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Wananchi wana matumaini makubwa sana na ninyi ,wamewaamini ,wakaja kwenye kampeni wakawapigia kura kuwachagua , msiende kuweka mikono mbele baada ya wananchi kuwapa dhamana hii, kwasababu ridhaa ya kuongoza kwenu kumetokana na wananchi na hao ndio waajiri wenu, mkawaheshimu” amesema Mhe.Batenga
Mhe Batemga ameongeza kuwa mafunzo kwa wenyeviti wa Vijiji , Vitongoji na Wajumbe wa serikali z a Vijiji yamelenga kuwapa nyenzo na kuwajengea uwezo ili waweze kujua majukum yao na namna ya kwenda kuyatekeleza kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kujenga Imani kwa Wananchi waliowaamini na kuwachagua
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Charles Jokery ametoa rai kwa viongozi hao wa Vijiji,Vitongoji na Wajumbe wa serikali za Vijiji kwenda kuwatumukia wananchi badala ya kuwa kero kwa wananchi kwani chama hakitasita kuwachukulia hatua wale wote watakao kuwa kero kwa Wananchi
“ Viongozi wa Vijiji na Vitongoji mmechaguliwa kwenda kuwatumikia wananchi na sio kwenda kuwalarua wananchi ,nendeni mkatatue kero za wananchi na sio kuongeza kero kwa wananchi , kumekuwa na tabia ya watu baada ya kuchaguliwa manakuwa kero na tishio kwa wananchi hiyo siyo dhamira ya chama cha Mapinduzi “ amesema Jokery
Naye katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndugu Yohana Mpamba amewaasa viongozi wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa serikali za Vijiji kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia misingi yote ya haki, sheria na taratibu za nchi zinavyosema kwani wao ndio waliobeba dhamana ya kuwatumikia wananchi katika maeneo yao .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chuya ndugu Cuthberth Mwinuka amewataka Viongozi wa vijiji kwenda kuhimiza wananchi kulima vizuri na kuyatunza mazao hayo kwani wakilima vizuri kijiji kitaepuka na janga la njaa lakini pia wataweza kuuza ziada ya mazao yao kwaajili ya kujipatia mahitaji mengine .
“Himizeni wananchi walime kwasababu ukijenga uchumi wa kijiji ndio maendeleo ya Kijiji, mimi sitarajii kuja kumuomba Mhe. Mkuu wa Wilaya aniletee mahindi kwaajili ya kusambaza kwa wananchi kwaajili ya njaa, chakula tunacholima ni chakutosha , tuhifadhi na ziada tuuze pasipo kusababisha njaa ndani ya familia. “ amesema Mwinuka
Wakizungumza kwa niaba ya viongozi wengine walipaota mafunzo wakati wa semina kwa Vijiji , Vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji Bi Rukia Mwakyusa ,Titho Kitema wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata yana umuhimu mkubwa sana kwao kwani yamewasaidia kujua mipaka yao pamoja na majukumu yao na mambo mbalimbali ya kwenda kuwaelimisha wananchi katika maeneo yao
Mafunzo kwa wenyeviti wa Vijiji , Vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji yamefanyika kwa makundi mawili kundi la kwanza ilikuwa tarafa ya Kipembawe Tarehe 8/12/2024 na kundi la pili Tarafa ya Kiwanja Tarehe 9/12/2024 yameenda sambamba na kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaj Batenga akiongea juu ya matumaini waliyonayo wananchi kwa Viongozi wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji wakati wa Mafunzo kwa Viongozi hao yaliyoenda sambamba na kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya ndugu Charles Jokery akitoa salam za Chama wakati wa mafunzo ya Viongozi wapya wa Vijiji,Vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri wa Sapanjo
Kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Cuthberth Mwinuka akiwataka Viongozi wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa serikali za Vijiji akiwasisitiza viongozi hao kuwahimiza wananchi waokulima vizuri ili waweze kupata mavuno mengi
Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Moses Ngole akifundisha juu ya majukum ya wenyeviti wa Vijiji,Vitingoji na wajumbe wa serikali za Vijiji wakati wa mafunzo yaliyofanyika kwa Viongozi wa Tarafa ya Kiwanja
Viongozi wa Vijiji, Vitongoji,na wajumbe wa serikali za vijiji wakiendelea kufuatilia mafunzo juu ya mada mbalimbali zilizofundishwa kwaajili ya kuwasaidia katika kutekeleza majukum yao
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.