Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simon Mayala amewataka wanafunzi na wanachunya kwa ujumla kubadili namna ya ulaji wa vyakula ili kuepukana na changamoto mbalimbali zinazotokana na ulaji mbaya, na kushauri umuhimu wa kuzingatia lishe bora huku akisisitiza kwamba lishe bora ni kupata mlo kamili na sio kushiba kama ilivyozoeleka kwa jamii nyingi ikiwepo wanafunzi ambao baadaye ndio Taifa la Kesho.
Hayo ameyasema leo 18/10/2023 kwa nyakati tofauti katika viwanja vya shule ya Sekondari Kiwanja na Shule ya sekondari ya kata Itewe alipokuwa akitoa elimu ya Lishe ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya lishe vijana balehe kitaifa yenye lengo la kutoa elimu ya lishe kwa vijana na namna bora ya ulaji unaozingatia afya.
‘’Lishe bora inaanza na namna ya ulaji kwani lishe bora sio kula na kushiba hivyo vijana kama taifa la kesho tunapaswa kuzingatia namna ya ulaji bora kutokana na changamoto mbalimbali za kiafya zinazotokana na ulaji mbaya kwani kumekuwa na wimbi kubwa la magonjwa ya moyo hii yote ni kutokana na vyakula tunavyo vitumia’’ alisema Mayala
Mayala ameongeza kuwa vijana wanapaswa kula kwa kuzingatia afya jambo ambalo litasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za kiafya kwa kutumia vyakula vinavyolinda mwili na kuwataka kuacha mara moja kula vyakula ambavyo vitawasababishia madhara ya kiafya kwa baadaye.
Naye Mkuu wa shule ya Sekodari Kiwanja Jackson Mnyalape amesema kuwa elimu ya lishe wanoyoipata wanafunzi ni muhimu kwa maisha yao ya sasa na hata maisha yao ya baadaye kwani itawasaidia hata kwa baadae watakapokuwa watu wazima na familia zao hivyo elimu hiyo ni muhimu sana kwao lakini pia watakuwa mabalozi wazuri hata watakapo rudi majumbani mwao.
Dorah Daniel, Isack Sajire kutoka shule ya sekondari kiwanja na Norberth Mawazo pamoja na Anastazia Ndede wa shule ya sekondari ya kata Itewe wamesema kuwa elimu ya lishe walioipata itawasaidia kupunguza au kuacha kula vyakula ambavyo vitawasababishia changomoto za kiafya kwa baadaye lakini pia upimaji wa hali ya lishe umewasaidia kujua hali zao za lishe na kujua wanatakiwa kufanya nini ili kuboresha zaidi hali zao za lishe.
Kampeni ya lishe vijana balehe yenye kauli mbiu ’Lishe kwa Vijana Balehe , Chachu ya Mafanikio yao”imehitimishwa rasmi leo tarehe 18/10/2023 katika halmashauri ya wilaya ya Chunya, na ilianza tarehe 16/10/2023. Kampeni imefikia Shule za sekondari Isenyela, Kiwanja na Itewe ambapo wanafunzi 756 wamepima hali zao za Lishe wakati wa Kampeni hiyo, Kampeni hiyo imehusisha Maafisa elimu Sekondari Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Wauuguzi kutoka hospitali ya Wilaya ,walimu pamoja na Wanafunzi
Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simon Mayala akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya Lishe kwa wanafunzi hasa Rika Balehe, Hapo ni shule ya Sekondari Kiwanja
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kata Itewe wakiwa katika utulivu wakati wakipatiwa elimu ya Lishe na Maafisa toka ofisi za elimu, na wataalamu wa lishe
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja wakipata elimu ya Lishe kutoka kwa wataalamu wa Lishe
Wataalamu wa Lishe kutoka Halmashauri ya wilaya Chunya wakishirikiana na wanafunzi kupima urefu wao na uzito ili kutathimini hali ya lishe
Kazi ikiendelea ya upimaji wa urefu sambamba na uzito ili kutathimini hali ya lishe kwa mlengwa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.