Chunya
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa walimu Taifa Oliver Mhaiki amewata walimu wilayani hapa kuwa wazalendo,kwa kutenda matendo yaliyo mema kwenye jamii inayowazunguka na wanafunzi wanaowafundisha ili kuendana na dhana ya Ualimu.
Mhaiki aliyasema haya wakati akizungumza na wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na waratibu Elimu kata, katika ziara yake ya kutembelea walimu mkoani Mbeya ambayo ameinzia katika Halmshauri ya wilaya Chunya ikiwa na lengo la kukumbusha majukumu ya walimu pamoja na waajiri ili kuhakikisha adhma ya Serikali ya kuanzisha Chombo hicho inatimia na Elimu bora inatolewa kwa wakati na ufanishi kwa watoto.
Alisema Tume ya utumishi wa walimu kama chombo kinachotambulika kitaifa kilianzishwa kwa nia ya kuwasaidia walimu, hii ni kutokana na wingi walionao ambapo asilimia 60 ya wafanyakazi wote nchini ni walimu.
Aidha aliwasihi walimu kuhakikisha wanawajibika kwa nafasi zao na mwajiri kuhakikisha Walimu wanatoa huduma kwa ufanisi, weledi na kwa wakati ili Elimu bora iendelee kutolewa kwa watoto kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aidha alisisitiza suala la kujituma na ushirikiano kati ya Walimu na waajiri pamoja na mamlaka za nidhamu ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa unyenyevu ili kuinua kiwango cha Elimu nchini.
Aidha ofisa Elimu mkoa Paulina Ndigeza akizungumza katika kikao hicho aliwapongeza walimu kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa walimu ambayo alidai inaendelea kufanyiwa kazi kwani si muda mrefu Serikali itaajiri walimu wapya.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Taifa Oliver Mhaiki akizungumza na walimu wilayani Chunya kuhusu Maadili ya Utumishi bora.
Afisa Elimu Mkoa Bi. Paulina Ndigeza akizungumza na Walimu wilayani Chunya.
Baadhi ya walimu wakiwa wametulia wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa tume ya utumishi wa walimu wakati akiwakumbusha maadili ya utumishi wa umma
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Bosco Mwanginde akiwasihi walimu kuzingatia mambo yote walioelekezwa.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.