WAKUUwa Idara, vitengo, pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji wa Halmashauri yaWilaya ya Chunya wamepatiwa mafunzo ya kuimarisha Utawala bora naUshirikishwaji wa Wananchi.
Mafunzohayo yametolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta zaUmma ujulikanao kama PublicSector Systems Strengthening, (PS3+) katika ukumbi wa mikutanowa Halmashauri.
Akizinduasemina hiyo Bw, Nazar Sola ambaye ni Mtaalamu wa kamati ya Mkoa mamlaka yaserkali za Mitaa, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha Wakuu wa Idara,Vitengo pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji kuweza kuratibu shughulizinazohusu ushirikishwaji wa wananchi katika masuala mbalimbali ya utawalabora, mipango na bajeti katika ngazi mbalimbali, hivyo kupitia mafunzo hayoyatawajengea uwezo watumishi wa ngazi zote kufanya kazi zao vizuri kwa mujibuwa sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali.
Aidha,amesisitiza juu ya matumizi ya tovuti na vyombo vingine vya mawasilianovinavyopatikana katika Hamashauri ya Chunya vitumike ipasavyo katikakuhabarisha umma juu ya matukio na masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii nakisiasa.
Watendaji wa Kata na Vijiji wakiwa kwenye Semina ya Kuimaisha Utawala bora na Ushirikishwashi wa Wananchi.
Bw. Nazar Sola Mtaalamu wa kamati ya Mkoa mamlaka ya serkali za Mitaa Akitoa Semina kwa Wakuu wa Idara, Vitengo na Watendaji wa Kata na Vijiji
Wakuu wa Idara Pamoja na Watendaji Wakiwa kwenye Semina ya Kuimarisha Utawala bora na Ushirikishwaji wa Wananchi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.