Wakuu wa Idara, Vitengo na Maafisa Bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wamepatiwa Mafunzo ya Mfumo wa Mpango na Bajeti (PLANREP) Ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Utekelezaji wa Shughuli ya kuandaa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2022/2023.
Mafunzo hayo yamefanyika Leo tarehe 16/12/2021 Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, ambapo Washiriki wamepatiwa Mafunzo toka kwa Wataalamu wa Halmashauri kupitia Idara ya Mipango.
Aidha Mafunzo hayo yamelenga Kuwajengea Uwezo wakuu wa Idara, Vitengo na Maafisa Bajeti juu ya namna ambavyo wanapaswa kufanya Maandalizi ya Bajeti kwa Kuzingatia Miongozo mbalimbali inayohusika Katika Uandaaji wa Bajeti ya Halmashauri
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya tayari wameanza kufanya Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, lengo ikiwa ni kuhakikisha wanatekeleza shughuli hiyo muhimu kwa wakati ili kuepuka ucheleweshaji wa Bajeti hiyo jambo ambalo Lita athiri Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Maendeleo ndani ya Halmashauri.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa Fedha 2022/2023 wakifuatilia mafunzo hayo katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Pichani ni Bw. Nebart Gavu Afisa Mipango wa Halmashauri akiwasilisha Mada katika Mafunzo ya Maandalizi ya Mpango na Bajeti
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.