Mwenyekiti wa Halmashaui ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Said Mwanginde amewataka wadau wa maendeleo na Wananchi kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Mhe Rais katika kujenga, kulinda na kuiendeleleza miundombinu mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao na kufanya hivyo itaendelea kusaidia uimarishaji wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo Yao
Ametoa rai hiyo jana Jumamosi ya tarehe 27/1/2024 alipokuwa anazungumza na wananchi katika hafla ya kukabidhi Chumba kimoja cha darasa kilichojengwa na mdau wa Maendeleo ndugu Salmon J Chanzu katika Sule ya msingi ya Soweto iliyopo kata ya Kasanga Halmashauri ya wilaya ya Chunya
“Kujenga chumba cha Darasa kama alivyofanya ndugu Salmon sio kwamba anapesa nyingi sana, lakini ni uzalendo na kuipenda nchi yako hivyo wadau wengine wa maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya tuendelee kumuunga mkono Mhe Rais katika ujenzi wa Miundombinu mbalimbali hii itaendelea kuturahisishia upatikanaji wa huduma katika maeneo yetu” alisema Mwanginde
Aidha Mhe Mwanginde pamoja na kumshukuru mdau wa maendeleo kwa kujenga darasa hilo amewaagiza watendaji wote wa Serikali kuwashirikisha wadau wa maendeleo katika maeneo yao ili washiriki ipasavyo katika ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na inawezekana wadau wapo ntayari kushiriki katika maendeleo lakini sisi watendaji wa Serikali mnaweza kuwa kikwazo cha wadau kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo
Awali kabla ya kumkaribishwa Mwenyekiti wa Halmashauri aliyekuwa mgeni rasmi katika Hafla hiyo Diwani wa kata ya Kasanga Mhe Benson Msomba amemshukuru mdau wa maendeleo kujenga Chumba cha darasa katika Shule ya Msingi Soweto na ameendelea kuhimiza wananchi na watu wote waliopo katika kata ya Kasanga kuendelea kuishi vizuri na wadau wa maendeleo jambo linaloleta matokeo chanya kama kuongezewa nguvu katika jitihada za maendeleo
Awali akisoma Risala ya kijiji cha Soweto kwa mgeni rasmi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Soweto mwalimu Mtalege Mwakalobo Classford alisema bado wanaupungufu wa Chumba kimoja cha darasa ambapo mpaka sasa wanaendelea kukusanya Fursa ili taratibu za ujenzi wa Chumba hicho cha Darasa uanze mapema lakini pia alimshukuru mdau wa maendeleo kwa kujenga Chumba hicho ambacho kitasaidia wanafunzi 45 wa darasa la awali katika shule hiyo na kupunguza idadi ya wanafunzi wengi kwenye chumba kimoja
Shule ya Msingi Soweto ina jumla ya wanafunzi 350 ambapo Chumba kilichojengwa kitapunguza upungufu wa vyumba viwili uliokuwa unaikabili shule hiyo ambapo upungufu wa chumba kimoja kinachobaki kwasasa fursa zinaendelea kukusanywa ili taratibu za ujenzi zianze mara moja hatimaye kuepukana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa kabisa katika shule hiyo.
Viongozi Mbalimbali wakimshukuru Mdau wa Maendeleo ndugu Salmon Chanzu baada ya kufungua rasmi chumba cha Darasa alichojenga kwenye Shule ya Msingi Soweto
Cheti ya pongezi kilichotolewa na uongozi wa kata ya Kasanga kwa Mdau wa Maendeleo ndugu Salmon Chanzu ikiwa ni ishara ya kutambua na kuthamini mchango wa mdau huo katika maendeleo ya kata hiyo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.