Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Bi Marietha Mlozi amewataka wadau wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuzingatia mambo muhimu yatakayowasaidia katika utekelezaji wa shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa za robo za utekelezaji wa shughuli zao katika idara husika, ushiriki wa wadau hao katika vikao mbalimbali, kulipa ada za kila mwaka na mambo mengine mengi.
Kikao hicho cha wadau kimeketi leo Tarehe 22/01/2025 katika Ukumbi wa mikutano wa Omary City Wilayani Chunya na kuhusisha wadau mbalimbali wanaotekeleza miradi ya afya na maendeleo kwa vijana kimeandaliwa na shirika la DSW linalotekeleza mradi wa afya na maendeleo kwa vijana(REST) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Wadau hao wa mashirika yasiyokuwa ya kiserkali wanaotekeleza miradi ya afya na maendeleo ya vijana wamekutana na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwasilishwaji wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na mashirika hayo kwa lengo la kufahamiana , pamoja na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukum yao.
Naye Mkurugezi wa Shirika la DSW ndugu Peter Owaga mbali na kuelezea shirika hilo, ameeleza pia shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika maradi wa afya na maendeleo ya vijana (REST) huku akiwataka wadau wanaotekeleza miradi ya afya na maendeleo kwa vijna kuendelea kushirikiana ili kumuwezesha na kumsaidia kijana kubaki salama ikiwa ni pamoja na kujitambua katika masuala mazima ya afya ya uzazi, pamoja na kujikwamua kiuchumi.
“Ndugu wadau leo tumefahamiana na kujua kila mmoja wetu kazi anazofanya na maeneo anayofanya kazi, hivyo sisi kama wadau tunaweza kuona namna gani tunaweza kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli zetu kwa maeneo yale ambayo tunatekeleza mradi , sambamba na hilo tunaweza kushirikiana hata katika maandiko mbalimbali kwasababu kazi yetu kubwa kama wadau ni kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.”amesema Owaga.
Aidha, wadau hao wamewasilisha shughuli mbalimbali wanazofanya ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ,uwezeshaji wa vijana kiuchumi , elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya magonjwa ya ngono na mambo mengine mengi yanayolenga kutatua changamoto katika jamii hususani kwa vijana ambao ni taifa la leo na kesho.
Kikao kazi cha wadau wanaotekeleza miradi ya afya na maendeleo ya Vijana kimewahusiaha wadau wa mashirika mbalimbali yanayotekeleza miradi yake katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya, mashirika hayo ni pamoja na shirika la DSW,HJMFRI,TDFT,PASADA,PHEDEA, Tasnema, Prospering for mind and window for Justice kwa lengo la kufahamiana na kuweka mipangokazi itakayo endelea kuwakutanisha wadau hao pamoja.
Mkurugenzi wa shirika la DSW Ndugu Peter Owaga akizungumza na wadau wanaotekeleza miradi ya afya na maendeeo ya Vijana namna ya kuendeleza ushirikiano wao katika kutatua changamoto mbalimali za vijana katika jamii wakati wa kikao kazi na wadau hao kilichoketi ukumbi wa mikutano wa Omary City Wilayani Chunya.
Mratibu wa mradi wa Afya na maendeleo ya vijana (REST) Bi celina Protas akielezea shughuli zilizotekelezwa kupitia mradi huo wakati wa kikao kazi na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika Ukumbi wa mikutano wa Omary City Wilayani Chunya.
Afisa Maendeleo ya jamii Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu James Sunge akiwakumbusha wadau juu ya usajili na wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wakati wa kikao kazi cha wadau wa afya na maendeleo ya vijana kilichefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Omary City Wilayani Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.