Afisa Mwandikishaji Jimbo la Lupa Wilayani Chunya Wakili Athumani Bamba amefanya kikao na viongozi wa vyama vya siasa kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajulisha juu za zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura kwani vyama vya siasa ni wadau wa kubwa wa zoezi hilo ili waweze kusaidia kuhamasisha jamii kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpiga kura
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Uchaguzi jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Leo Tarehe 21/12/2024 ambapo Viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa Wilaya ya Chunya wameshiriki
“Zoezi la uandikishaji litaanza rasmi tarehe 27/12/2024 hivyo lengo la kikao hichi ni kuwapa taarifa ninyi kama viongozi wa vyama vya sias kwasababu tunajua mnamtaji mkubwa wa watu hivyo mtatusaidia kuhamasisha na kuwajulisha Wananchi juu Ya zoezi la kujiandikisha pamoja na kupeleka Mawakala wenu katika vituo vya kujiandikishia”
Aidha Afisa mwandikishaji jimbo la Lupa ameongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo Wilayani Chunya kwaajili ya kuhakikisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura linafanyika kwa ukamilifu kwani zoezi hilo limeeanza na utolewaji wa Mafunzo kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata na mafunzo hayo yataendelea kwa wahusika wengine wa zoezi hilo pamoja na kuapishwa kwa Mawakala wa vyama vya siasa
Naye Afisa Uchaguzi Wilaya ya Chunya ndugu Ridhiwani Mshighati amesema kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari la Mpiga kura litahusisha watu ambao wamehama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, wale waliokuwa hawajafikisha umri wa kujiandikisha na sasa wamefikisha umri wa kujiandikisha lakini pia kuondoa taarifa za watu waliofariki na sifa zingine ambazo zimeainishwa .
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Charles Jokery, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndugu Yohana Mpamba na Mwenyekiti wa ACT wazalendo ndugu Timoth Mwafumu wametoa mapendekezo yao juu ya ratiba iliyotolewa ya kuwaapisha Mawakala lakini pia kupanga vituo kulingana na jographia ya Chunya jinsi ilivyo ili kuwarahisishia na kuwapunguzia adha mbalimbali Mawakala wa vyama vya siasa
Kikao cha Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa na Viongozi wa Vyama vya siasa kimehudhuriwa na Afisa Mwandikishaji Jimbo, Afisa Uchaguzi, Viongozi kutoka vyama viNNE vya siasa ambavyo ni CCM, CHADEMA , ACT wazalendo, CHAUMMA na Balaza la Wanawake Chadema (BAWACHA) na kujadili mambo mbalimbali kuhusu zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la Mpiga kura ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi Mkuu Octoba 2025
Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa wakili Athuman Bamba akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa juu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura
Afisa Uchaguzi Wilaya ya Chunya ndugu Ridhiwani Mshigati akizungumza sifa za watu wanaopaswa kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpiga kura
Katibu wa Chama cha Demokrsia na Maendeleo Chadema ndugu Yahana Mpamba akitoa mapendekezo wakati wa kikao cha Afisa mwandikishaji Jimbo la Lupa na vyama viongozi wa vyama vya siasa .
Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa watatu kutoka kulia kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa Wilaya ya Chunya baada ya kumaliza kikao
Viongozi wa vyama vya siasa Wilayani Chunya wakisikiliza lengo la kikako kutoka kwa Afisa Mwandikishaji Jimbo la Lupa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.