MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Said Mwanginde amewataka vijana wilayani chunya kukopa fedha zinazotengwa kutoka kwenye mapato ya ndani ili kurahisisha shughuli zao za kujikwamua kiuchumi kwani fedha zipo huku akisema jambo muhimu ni kutimiza vigezo
Mhe, Mwanginde amesema hayo leo wakati akikabidhi basi Moja (1) kwa kikundi cha Champions group kutoka kata ya Chokaa ambalo limenunuliwa kutokana na fedha za asilimia kumi (10) zinazotengwa na halmashauri kwaajili ya Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu
“Vijana hii gari ni yakwenu mamlaka yote yapo chini yenu sisi kama halmashauri kazi yetu ni kusimamia marejesho mnapopata kiasi cha fedha mrejeshe ili tufanye utaratibu wa kukopesha vikundi vingine” amesema Mwanginde
Viongozi wa vikundi vya vijana kutoka kata hizo wameeleza namna walivyopokea mabasi hayo huku wakiishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasaan kwa mikopo hiyo na kuwahimiza vijana wenzao kuunda vikundi ili waweze kukopesheka
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Chunya Bi. Ester Kondobole ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu mikopo ya fedha zinazotengwa kutoka makusanyo ya ndani huku akisema milioni 50 zilizotengwa kwaajili ya makundi ya watu wenye ulemevu zipo kwakuwa hakuna kikundi chochote kilicholeta maombi ya kukopeshwa fedha
“Kuna fedha miloni 50 ambazo zilitengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu zipo na bado hazijatolewa kwani hakuna kikundi chochote kilicho leta maombi” amesema Bi. Ester Kondobole
Bi. Kondobole amefafanua Zaidi kuwa vikundi vya wanawake wilayani humo vimefaidika pia na mikopo hiyo ya asilimia kumi (10) za mapato ya ndani kwa kukopeshwa milioni hamsini na tano (55)
Serikali imekuwa ikizitaka halmashauri kutenga asilimia kumi za mapato ya ndani kwaajili ya kuwakopesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuboresha maisha yao wenyewe na familia zao
Makabidhiano hayo leo ilikuwa ni kuhitimisha zoezi lililoanza mapema mwezi January 2023 ambapo basi moja lilipokelewa na halmashauri kwa ajili ya kikundi cha Winners group kutoka kata ya Itewe.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde wakwanza kushoto akimkabizi kadi ya gari kwa mwenyekiti wa kikundi cha Champions group Ndg Denis Mwalukuga ambaye aliongozana na Mtunza hazina wa kikundi hicho Bi. Hadija Ngemelo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.