Vijana Vinara kupitia mradi wa afya na maendeleo ya Vijana (REST) unaotekelezwa na shirika la DSW wamejengewa uwezo juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ikiwa ni pamoja na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu, pamoja na mikopo ya wajasiriamali wadogo au machinga ili kuwawezesha vijana kujiajiri pamoja na kujipatia kipato kitakachowawezesha kujipatia kipato kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kuchangia katika kuinua uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Fursa hizo zimeelezwa na Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi leo tarehe 21/01/2025 wakati wa kikao cha ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mradi wa REST kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Omary City Wilayani Chunya.
“Serikali yetu ina fursa kwaajili ya vijana kwahiyo niliona ni vizuri hadhara hii itambue fursa hizo, kwanza tuna mikopo ya yasilimia 10% kwaajili ya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu lakini pia mikopo ya wamachinga au wajasiriamali wadogo kwani mbali na kufanya shunguli za mradi ni vizuri makafahamu fursa zilizopo muweze kuzitumia lakini pia muweze kuwa mabalozi wazuri kwa vijana wengine kule mnakotoka”. Amesema Mlozi
Aidha Bi Marietha emewaeleza vijana hao vitu muhimu vya kuzingatia ili vijana waweze kupata fursa hizo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi, kusajili kikundi lakini pia wajumbe watatakiwa kuwa na namba za nida pamoja na muhitasari wa kikundi na mambo mengine ili kuweza kukidhi vigezo vya kupata mkopo pamoja na fursa zingine.
Awali akizungumza mbele ya wajumbe Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la DSW linalotekeleza mradi wa afya na Maendeleo ya Vijana ndugu Peter Owaga amesema mbali na kufanya ufuatiliaji na thinini ya hali ya utekelezaji, vijana vinara wamejengewa uwezo juu ya namna ya kuandaa mpango kazi utakao wasaidia katika utekelezaji wa shughuli zao katika jamii pamoja na kufikia malengo ya mradi
Aidha Owaga amewataka vijana vinara wa mradi kuhakikisha mambo mbalimbali waliyojifunza ikiwa ni pamoja na kuwezeshwa kuzitambua fursa mbalimbaliza, mikopo kwa vijana na mambo mengine, kuhakikisha elimu hiyo inawafikia na watu wengine wakiwepo vijana katika maeneo yao wanayotoka kwani moja ya kazi yao ni kufikisha elimu wanayoipata kutoka kwa shirika na wadau katika jamii yao.
Naye Afisa kutoka divisheni ya Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Elizabeth Lusale amewaeleza vijana juu ya uwepo wa Mkopo wa wajasiriamali wa dogo au wamachinga ambapo amesema kuwa kigezo kikubwa cha kupata mkopo huo ni kitambulisho cha ujasiriamali ambacho hutolewa na Halmashauri ya Chunya ambapo kima cha chini cha mkopo huo ni shilingi laki moja (100,000) na ukomo wa mkopo huo ni shilingi million nne (4,000,000).
Wakizungumza kwa niaba ya viajana vinara wengine ndugu Yohana Kilua, Rose mwalukasa kutoka kata ya Chokaa na Obed Elia kutoka kata ya Matundasi wameuliza juu ya watu wanaopaswa kuunda kikundi na endapo kikundi kimechukua mkopo alafu miongoni mwa wanakikundi wakawa wametangulia mbele za haki kunakuwa na utaratibu gani ambapo majibu ya maswali hayo yameweza kujibiwa na Maafisa Maendeleo ya jamii ili kuwajengea uelewa vijana hao.
Kikao cha Tathimini ya mradi wa Afya na maendeleo ya Vijana (REST) unaotekelezwa na shirika la DSW kimehusisha wadau wanaotekeleza Miradi katika maeneo tofauti tofauti, wafanyakazi kutoka shirika la DSW, na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya pamoja na vijana vinara kutoka kata sita (6) za mradi ambazo ni Matundasi, Makongolosi, Lupa, Mafyeko, Choka na Sangambi. Kikao hicho kimeenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya michezo ambavyo ni jezi na mipira kwa vijana vinara
Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Marietha Mlozi akielezea uwepo wa fursa mbalimbali kwa vijana wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji kupitia mrari wa afya na maendeleo kwa vijana REST kilichoketi ukumbi wa Omary City.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la DSW akizungumza na vijana Vinara wa mradi juu ya ya hali ya utekelezaji wa shughuli za mradi wakati wa kikao cha tathimini kilichofanyika Ukumbi wa Omary City Uliopo Wilaya ya Chunya.
Yohana Kilua kutoka kata ya Chokaa akiuliza swali kwa afisa maendeleo ya jamii ili kuoneza uelewa juu ya fursa mbalimbali walizoelekezwa kwaniaba ya vijana vinara wengine.
Vijana vinara wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya wakiwa wamevaa jezi zao walizokabidhiwa na mipira kutoka shirika la DSW.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.