Mradi wa Afya na maendeleo ya vijana (REST) unaotekelezwa na shirika la DSW Tanzania katika Hammashauri ya Wilaya ya Chunya unalenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana ikiwa ni pamoja na Afya ya Uzazi, ukatili wa kijinsia na changamoto pamoja na kuwawezesha vijana kiuchumi ili kuweza kujitambua , kulinda Afya zao na kujitegemea kiuchumi.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Shirika la DSW-Tanzania, ndugu Peter Owaga Desemba 5, 2024 wakati wa mafunzo kwa vijana vinara ili waweze kuwajengea uwezo vijana wenzao pamoja na kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao kwa kushirikiana na serikali.
Awali akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mwl. Costansia Komba amesema kuwa Halmashauri wako tayari kuyafanyia kazi yale yote yatakayohitaji kufanyiwa kazi huku akiwataka vijana washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika maeneo yao ili kutimiza adhima ya mradi wa REST ya kuwasaidia vijana katika afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia,pamoja na kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la DSW Tanzania ndugu Peter Owaga amesema kuwa shirika linatekeleza miradi mbalimbali ya afua za afya na maendeleo kwa vijani ili kuona kijana ni mtu mwenye manufaa katika jamii ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vijana kijitambua kwenye masuala ya afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia , stadi za maisha na uongozi pamoja na kuwahimiza kushiriki kwenye miradi ya maendeleo.
“ Kwenye huu mradi wa REST kazi yetu kubwa itakuwa ni kuimarisha uwezo wa Vijana Vinara ambao wametambuliwa na serikali kwaajili kuwajengea uwezo kwaajili ya kuwafikia vijana wengine ikiwa ni pamoja kuhimiza ushiriki wao katika shughuli za maendeleo, kuimarisha stadi za maisha na uongozi” alisema Owaga.
Aidha Owaga ameongeza kuwa, mradi wa REST unalenga kuimarisha mifumo iliyopo, kujenga uwezo wa wataalam waliopo ili kutokomeza ukatili wa kijinsia, kuimarisha upatikanaji wa huduma rafiki kwa vijana pamoja na kuhakikisha sauti za vijana zinakuwa mstari wa mbele kuibua changamoto za vijana na kuzitafutia ufumbuzi .
Afisa Maendeleo vijana Wilaya ya Chunya ndugu James Sunge amesema kuwa vijana wengi wamekuwa na changamoto nyingi kama vile mimba za utotoni , uonjwa wa UKIMWI , ukatili wa kijinsia na changomoto zingine zinazochagizwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa madini hivyo ujio wa mradi wa REST kutoka shirika la DSW utasaidia kuzitatua na kuzipunguza changamoto hizo.
Akiongea kwa niaba ya wawezeshashi mwezeshaji wa Kitaifa Huduma rafiki kwa Vijana bi Mariam Mhanjim amesema, shirika la DSW wanawawezesha vijana vinara ili kuwasaidia vijana wengine kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu juu ya changamoto mbalimbali za Afya hivyo vijana kinara watawasaidia viajana wengine waweze kufika kwanye vituo vya Afya kwaajili ya kupata huduma au kuwapa huduma wanapofika katika vituo vya Afya ili kuwawezesha vijana kuvuka wakiwa salama.
Wakiwawakilisha vijana wengine waliopata mafunzo REST, ndugu Samuel Macha Mtoa huduma za afya na ndugu Ngugu Joseph Kasota, Mtoa huduma za Afya ngazi ya jamii wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kuwaelimisha vijana na kuwasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya na changamoto zingine ili kijana aweze kujua njia sahihi na salama za kujikinga na kuvuka ujana akiwa salama lakini pia kujitambua kama kijana ni nguvu kazi ya taifa.
Mradi wa REST unaotekelezwa na shirika la DSW-Tanzania unatekelezwa katika kata 6 ambazo ni kata ya Mafyeko,Lupa, Makongolosi, Matundasi,Chokaa na Sangambi za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika tarafa ya Kiwanja na Kipembawe yamehudhuriwa na Watoa huduma za Afya kutoka katika vituo vya kutolea huduma za Afya, Watoa Huduma za Afya ngazi ya jamii, Afisa Maendeleo vijana , Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Chunya na Walimu kutoka shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Chunya.
.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mwl. Costansia Komba akifungua mafunzo yanayotaolewa na Shirika DSW- Tanzania kupitia mradi wa REST unaotekelezwa kwenye kata sita katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Mkurugenzi waShirika la DSW -Tanzania akizungumza na Vijana vinara kutoka kata 6 za mradi wakati wa mafunzo yaliyotolewa Ukumbi wa Omary City katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya
w
Wallimu wa shule za msingi na Shile za Sekondari wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la DSW-Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Omary City katika Hamlmashauri ya Wilaya ya Chunya
Watoa huduma za Afya wakiwa kwenye picha na wafanyakazi wa shirika la DSW-Tanzania baada ya kutoka kwenye mafunzo Ukumbi wa Omary City
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.