Mkuu wa wilaya ya Chunya Mheshimiwa MarryPrisca Mahundi leo amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo. Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri (Sapanjo Hall) ambapo aliwakabidhi vitambulisho baadhi ya wajasiriamali kwa niaba ya wote.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya aliwaeleza wajasiamali hao kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli anawajali na ndio maana ameamua kuwapatia hivyo vitambulisho ili iwasaidie kufanya biashara zao bila usumbufu wowote na kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadaye.
wafanyabishara wadogo wadogo katika zoezi la uzinduzi na uchukuaji wa vitambulisho
Kigezo cha kupata kitambulisho hicho cha ujasiriamali ni kuwa na mtaji usiozidi shilingi milioni nne za kitanzania (4,000,000) na mauzo yako hayazidi shilingi elfu kumina mbili na mia tano za kitanzania kwa siku (12,500)
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya aliwataka wafanyabiashara hao wadogo kutokutumia vitambulisho hivyo kwenda kinyume na sharia zilizopo ikiwa ni pamojana kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa. Mjasiriamali atatakiwa kuvaa kitambulisho hicho awapo eneo lake la biashara na asimpe mtu mwingine yeyote ili kuepuka usumbufu kwa watu wa mamlaka ya mapato Tanzania (T.R.A).
Mheshimiwa MarryPrisca Mahundi akiwahusia wafanyabiashara wadogowadogo Chunya
Pia aliwataka wafanyabiashara hao kulipia kiasi cha shilingi elfu ishirini tu kama gharama ya kutengeneza vitambulisho hivyo.
Katika upande mwingine Mheshimiwa mkuu wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwatakia wananchi wote wa Halmashuri ya Chunya heri ya mwaka mpya 2019 na washerehekee wa amani na upendo bila kuvunja sheria za nchi.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.