Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndg Albert Chalamila leo siku ya Alhamisi Tarehe 4/4/2019 katika ukumbi wa Mkapa uliopo jijini Mbeya amezindua rasmi mfuko wa bima ya Afya iliyoboreshwa.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa mkoa amesisitiza Halmashauri zote kuhakikisha zoezi hili jema linatekelezwa kwa asilimia mia moja kwani ni ndoto na shauku kubwa ya
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Joseph Pombe Mgufuli kuona wananchi wote wanapata huduma bora ya Afya.
Katika uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa pia na Wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya, Wenyeviti wa Halmshauri, Wakurugenzi Watendaji, waratibu wa
ICHF (IMPROVED COMMUNITY HEALTH FUND), Maafisa TEHAMA wilaya, waganga wakuu wa wilaya, Mkuu wa mkoa ameagiza elimu ya kutosha itolewa
kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya Afya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.