Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia kwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) Mhe Bosco Mwanginde ametangaza kiama kwa Watumishi wasimamizi wazembe wa Miradi na Mafundi wazembe katika utekelezaji na usimamizi wa miradi jambo ambalo linapunguza ubora na kasi ya utekelezaji wa miradi hivyo kuleta mashaka kwa wananchi na Serikali yao
Akizungmza wakati akijumuisha lengo la ziara ya kamati hiyo iliyofanyika siku mbili tarehe 3/1/2025 na 4/1/2025 amesema Baraza la Madiwani halitavumilia kuona miradi inasimamiwa vibaya na Mafundi hawatunzi na kutumia vizuri vifaa vya ujenzi
“Kamati imebaini usimamizi mbaya kwenye ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi Isangawana hivyo imeagiza Shimo libomolewe na lianze kujengwa upya huku Kamati ikiagiza Jengo la vyoo hivyo lipigwe upya plasta Chini ya Gharama na usimamizi wa Mhandisi maana yeye ndiye aliyesababisha ujenzi huo kuwa chini ya viwango hivyo kamati imeagiza atatoa gharama za marekebisho hayo ndani ya wiki tatu” Alisema Mhe Mwanginde
Aidha, Kamati hiyo imepongeza utekeleaji wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya kata Nkung’ungu ikiwataka wananchi wa vijiji vyote kuhakikisha wanashiriki ipasavyo maeneo yanayohitaji nguvu kazi yao kwani Lengo la Serikali ni kufunguliwa kwa shule hiyo mapema iwezekanavyo ili kuwaepusha wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya Shule
Mhe Tusalim Mwaijande, Mhe Sailon Mbalawata, Mhe Kimo Choga, Mhe Phide Mwalukasa, Mhe Rehema Kifwamba, Mhe Samweli Komba na Mhe Haji Chapa pamoja na Ushauri walioutoa maeneo mbalimbali wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kuendelea kuleta fedha kwenye Halmashauri ya wilaya ya Chunya jambo ambalo litaendelea kuondoa adha kwa wananchi wa Chunya kwani huduma zote zitapatikana kwa weledi na kwa wakati
Ziara ya kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imedumu kwa siku mbili na imekagua miradi mbalimbali ikiwepo Ujenzi wa Mabweni kwa shule za Sekondari Sangambi, Isenyela na Makongolosi, Ujenzi wa Stendi Mpya ya Mabasi, Ujenzi wa Uwanja wa Michezo, Ujenzi wa vyoo na tanki la maji Zahanati ya Bitimanyanga, Ujenzi wa Bwalo la Chakula Shule ya Sekondari Lupa na baadaye kukamilisha ziara kwakukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule Mpya ya kata ya Nkung’ungu
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakishauriana wakati wakitazama Shimo la Choo lililojengwa chini ya kiwango katika Shule ya Msingi Isangawana wakati wa ziara yao ya kawaida ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa ndani ya wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.