Afisa utumishi na rasilimali watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu John Maholani akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri amewataka wananchi kuendelea kufanya usafi wa mazingira wakati wote na ili kufanikisha hio ni lazima usafiwa mazingira iwe jadi yetu.
Kauli hiyo ameitoa 16/09/2023 wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya usafishaji duniani ambapo kwa halmashauri ya Wilaya ya Chunya wameadhimisha kwa kufanya usafi wa mazingira ya ndani na nje katika Soko la Uhindini lililopo kijiji cha Kibaoni kata ya Chokaaa.
Nae afisa mazingira wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Yohana Ngulukia amewataka wananchi kudumisha usafi wa mazingira kama sehemu ya maisha ya kila siku kwani mazingira yanapokuwa safi na afya zitakuwa salama lakini mazingira yanapokuwa machafu husababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali .
“Nawaomba wananchi tuzingatie sana usafi wa mazingira usafi iwe jadi yetu kwani usafi ni kinga na kinga ndio tiba ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu wa mazingira na usafi huu tulioufanya leo hapa uendelee kufanyika mara kwa mara”.
Aidha Ngulukia ameongeza kuwa Jukum la Usafi wa mazingira ni suala la kulizingatia na kulipakipaumbele kuanzia majumbani,katika taasisi na maeneo yanayotuzunguka hivyo ni vyema usafi uzingatiwe kwa kufwata utaratibu pasipo kusubiria kuchukuliwa hatua au kotozwa faini kwasababu ya kutokufanya usafi.
‘‘Twendee kufanya usafi hata majumbani kwetu mazingira bado hayaridhishi kila mtu awajibike kwa kufanya usafi wa mazingira , kuchimba mashimo ya taka na kuchoma taka ngumu pamoja na kusafisha mitaro inayotuzunguka tuifanye Chunya yetu iwe safi wakati wote.alisema Ngurukia”
Katibu wa Soko la Uhindini ndugu Metusela Kilawa kwa niaba ya wafanyabiashara wa soko hilo amewashukuru watumishi mbalimbali na wananchi waliojitokeze kufanya usafi sokoni hapo na kuahidi kuwa usafi wa mazingira sokoni hapo utaendelea kufanyika mara kwa mara.
Maadhimisho haya yameadhimishwa tarehe 16/09/2023 ya kiongozwa na kauli mbiu inayosema “Tuungane pamoja ,Kujifnza,Kupanga na Kuhimiza Uimarishaji Huduma za Udhibiti wa Taka”na yamehudhuriwa na watumishi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Chunya, viongozi wa dini, vyombo vya ulinzi na usalama, wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo.
Afisa Mazingira Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bw. Yohana Ngulukia amizungumza jambo na wananchi waliojitokeza katika zoezi la kuisafisha dunia Septemba 16, 2023
Wananchi pamoja na watumishi wakichoma taka baada ya kukusanya toka maeneo mbalilmbali ya soko la Uhindi katika siku ya kusafisha Dunia
Baadhi ya wananchi na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakisikiliza nasaha za Viongozi baada ya zoezi la kuisafisha Dunia kukamilika katika soko la Uhindi september 16, 2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.