Timu ya Tathimini ya zao la Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Chunya kupitia wataalamu Mbalimbali imewataka Vyama vya msingi vya Ushirika kuhakikisha wanaendelea kuhimiza na kuwasimamia wakulima katika upandaji na uhifadhi wa miti kwani ukaguzi wa miti iliyopandwa kwa mwaka jana na mwaka huo utafanyika mapema kabla ya ufunguzi wa masoko
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti katika vyama vya Nkung’ungu na Ifuma wawakilishi kutoka bodi ya Tumbaku, Chama kikuu cha ushirika Chunya CHUTCU pamoja na wadau wanaounda timu ya tathimini ya zao kwa mwaka 2024 wamesema kabla ya masoko kufunguliwa rasmi mapema mwezi Aprili ukaguzi wa miti iliyopandwa mwaka jana na mwaka huu utafanyika hivyo wamewataka viongozi wa bodi kuhakikisha wanachama wao wanatimiza takwa la kisheria kuhusu kilimo cha zao la Tumbaku.
“Kabla masoko hayajafunguliwa rasmi mwezi wa nne, kutakuwa na zoezi la ukaguzi wa miti iliyopandwa mwaka jana na mwaka huu, hivyo hakikisheni miti imepandwa na imetunzwa kwa mujibu wa taratibu zetu za kilimo cha Tumbaku..., Zingatieni taratibu, kanuni na miongozo ya Kilimo cha Tumbaku…, Tumbaku tuliyoiona endeleeni kuitunza ili tukaione pia kwenye Masoko hapo baadaye hivyo wasimamieni wakulima ili wafikie malengo”. Alisema Cleopa Nziku, Loysujaki Kimiri na Ahazi Itika
Aidha Cleopa Nziku kutoka Bodi ya Tumbaku mkoa wa Kitumbaku Chunya amewashauri wakulima kuzingatia ushauri na maoni yanayotolewa na timu ya Tathimini ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwahimiza wakulima kutunza tumbaku ili kupata Tumbaku yenye ubora kwakuwa zoezi la Tathimini huwa lina uhalisia sana hivyo wakizingatia ushauri wa timu nzima itawasaidia kufika malengo waliyojiwekea wao kama chama
"Zoezi hili huwa halidanganyi hivyo zingatieni ili kuhakikisha wanayafanyia kazi hayo mapendekezo ya Wajumbe wa watathimini na Msipofuata taratibu za kilimo cha Tumbaku tutawatoeni hivyo hakikisheni mnazingatia kutowashirikisha watoto kwenye kazi za kilimo cha Tumaku, Zingatieni kupanda miti na kuzingatia usalama kwa watu wanaofanyakazi Maeneo yenu” Aliongeza Bwana Nziku
Naye Ahazi Itika kutoka kampuni ya Kwawa Leaf Tobacco amewashauri viongozi wa vyama vya Msingi na bodi kwa ujumla kuhakikisha wanawasimamia wananchi kuchuma Tumbaku kwa wakati ili kuepuka upotevu ambao unaweza kuepukika maana kiwango tunachokiona ni kizuri na kitanatakiwa kusimamiwa ili masoko yatakapoanza tushuhudie hali nzuri tuliishuhudia tukiwa kwenye tathimini
Adili Juma, Ndakson msole na Chrispin Mpasula kwa niaba ya viongozi wengine wa bodi ya Chama cha Ushirika Nkung’ungu wanawashukuru timu nzima ya tathimini iliyofika kwenye chama hicho na kusema wamepokea maelekezo, ushauri na mapendekezo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kufikia makisiso ya kuzalisha kwa chama chao
Zoezi ya tathimini ya zao la Tumbaku linaendelea katika mkoa wa kitumbaku Chunya ikiwa ni siku yake ya nne ambapo timu zote mbili zikiendelea kufika katika mashamba ya wakulima kwakushirikiana na wajumbe wa bodi za vyama husika na kuona hali ilivyo na kutoa ushauri mbalimbali huku zoezi hilo likitegemewa kutoa makisio ya uzalishaji kwa msimu wa 2023/2024 tayari kuelekea ufunguzi wa masoko mapema mwezi wa nne
Mjumbe wa Chama Cha ushirika cha Nkung'ungu akichangia jambo mbele ya timu ya Tathimini ya zao la Tumbaku ilipopita kwenye Chama hicho na kufanya tathimini ya zao hilo
Timu ya Tathimini ya zao la Tumbaku ikifanya Majumuisho kwenye moja ya mashamba yaliyopitiwa wakati wa tathimini baada ya kumalizia kutembelea shamba hilo na kujionea hali ya uzalishaji
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.