Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh. Mayeka S. Mayeka amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kuhifadhi chakula cha kutosha familia zao ili kuepukana na mfumuko wa bei za vyakula kama ilivyokuwa mwaka huu, huku akiwakumbusha kuhakikisha wanachangia Chakula shuleni ili wanafunzi wawapo shuleni wapate chakula cha Mchana hatimaye wasome kwa utulivu.
Amesema hayo jana tarehe 7/6/2023 alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Soweto, kata ya Kasanga ambapo ilikuwa ni hitimisho ya ziara ya kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya iliyokagua miradi mbalimbalimbali ikiwepo Zahanati ya Everist, Daraja la Isenyela-Sangambi, Ujenzi wa Barabara ya Ifumbo, Ujenzi wa Nyumba ya walimu yenye uwezo wa kubeba familia tatu kwa wakati mmoja shule ya msingi Ifumbo pamoja na mradi wa maji ifumbo
“Hali ya Chakula safari hii haikuwa mbaya ukilinganisha na mwaka uliopita, Nataka niwaombe jambo moja, Sasa hivi tumevuna lakini chakula huwa hakitoshi, Niwaombe tutunze Chakula. Niwaombe pia tuchange chakula kwaajili ya watoto wetu wapate chakula shuleni kwani itawasaidia kusoma kwa bidii”
Wakati akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Soweto na wanachunya kwa ujumla wake Mhe. Mayeka amewahakikishia wananchi wa Chunya kwamba Changamoto za Mbolea zilizojitokeza Msimu huu tayari zimeshawekewa mikati na serikali ili zisijitokeze tena huku akionya wanachunya kutotumia vibaya Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2022 ambapo idadi ya wanaume imeonekana kuwa ni kubwa kuliko wanawake hivyo wasianze kuwaharibia wanafunzi wa kike masomo yao kwa kuwatongoza.
“Changamoto zote za Mbolea zilizojitokeza msimu uliopita zimeshachukuliwa na serikali na zimefanyiwa kazi tayari, na tayari utaratibu mzuri wa usimamizi wa Mbolea umeandaliwa, Mbolea itafika mapema na kwa usimamizi mzuri Lakini pia ni kweli sense imeonesha uchache wa wanawake wilayani Chunya lakini msitumie nafasi hiyo kuwatongoza wanafunzi kwani kwa kufanya hivyo mnaitafuta miaka thelasini (30) au kifungo cha Maisha jela”
Damas Lunda, Peter Mwakatiku na Sofia Ntongolo pamoja na kutoa shukrani zao kwa serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyowajali, waliwawakilisha wananchi wengine kutoa hoja mbalimbali ambazo zilipatiwa majibu na Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na wakuu wa Idara akiwepo Mhandisi Leon Kavishe kaimu meneja RUWASA, Mhandisi Senyange Kayora TARURA.
Awali akitoa salamu za kata ya Kasanga Diwani wa Kata hiyo Mhe Benson Msomba amesema mpaka sasa wapo katika hautua za ujenzi wa Msingi wa madarasa sita kwaajili ya kunaza shule ya sekondari ya kata hiyo ambapo kukamilika kwakwe itasaidia kupunguza umbali mrefu wa wanafunzi kutoka kata hiyo kufuata masomo katika kata nyingine (Kata ya Itewe) na Itapunguza utora kwa wanafunzi
Miradi yenye gharama ya zaidi ya bilioni moja na milioni mia tano (1,500,000,000/=) imetembelewa na kamati ya ulizni na usalama ikiwa ni kuhakikisha ukamilifu wake unakuwa wa kiwango tarajiwa huku gharama za miradi hiyo iendane na thamani ya fedha zilizotolewa jambo ambalo ndiyo kusudi la serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.