Mkuu wa wilaya ya chunya Mhe, Mbarak Alhaji Batenga amewataka wananchi wa Chunya kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania na Viongozi wake ili Amani iliyopo iendelee kudumu huku akiwasisitiza wananchi wote bila kujali dini na dheheubu Kulinda na kudumisha Amani jambo liotakalofanya tuendelee kujihusisha na shughuli za maendeleo na Jambo hilo linawezekana kwa njia ya Maombi kwa
Kauli hiyo ameitoa mapema leo tarehe 22.Aprili 2024 wakati wa dua na Maombi ya kuliombea Taifa katika maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo).
‘“Ili Amani iweze kupatikana lazima watu wakubali kutenda haki tusipotenda haki tunatafuta kuvuruga amani kama wewe ni mtumishi tenda haki katika nafasi yako ,ukiwa wewe ni mfanyabiashara tenda haki katika afasi hiyo ,tunapokuja kuliombea Taifa nasisi pia tujiombee kwasababu kama amani inavurugika sisi ndio tunaovuruga.’’alisema Batenga
Mwenyekiti jumuiya ya maridhiana ya Amani Wilaya ya Chunya Mch Anyandwile Kajange kutoka kanisa la Moraviani kwaniaba ya viongozi wa Dini zote amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Chunya pamoja na kwenedea kuilinda na kuidumisha Amani huku akiomba Serikali kuingilia kati Matumizi ya Mitandao ili kudhibiti mmomonyoko wa Maadili kwa Taifa.
Nao viongozi wa dini sheikh Abdulijalili Jambia na Fr Kanon Mapunda Mchungaji kutoka Kanisa la Angikana kwaniaba ya Viongozi wa dini wamewaongoza wanacnhi wa wilaya ya Chunya katika dua na maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania pamoja na viongozi wote ili kuendelea kudumisha amani na kuulinda Muungano pamoja na kuomba Mungu aliepushe Taifa dhidi ya majanga mbalimbali yanayoendelea kuikumba nchi ya Tanzania.
Awali akitoa salama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona amewapongeza wananchi wa Chunya kwa utulivu, ushiriki wao kwenye miradi ya maendeleo na kuwataka kwendelea kuilinda Amani iliyopo pamoja na kudumisha Muungano wa Tanzania.
“Niwashukuru Mkuu wa Wilaya,Viongozi wa Chama, viongozi wa dini mbalimbali ,waheshimiwa madiwani na wananchi kwa Ushirikino mkubwa mnaotupatia kama Halmashauri niwaombe ushirikiano huu mwendelee kuutoa lakini pia twendelea kuimarisha Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar kwani Muungano huu tulinao ndio unaotufanya twendelee kuishi kwa Amani bila ubaguzi wa aina yeyote.”alisema Kambona.
Ibada hiyo ya Dua na Maombi ya kuliombea Taifa yamefanyika leo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) ikiwa ni kelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, Ibada imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya , Wanafunzi pamoja na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya mhe. Mbarak Alhaj Batenga aliesimama katikati akiwa na viongozi wa dini pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumaliza Dua na Maombi ya kuliombea Taifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sapanjo wilayani Chunya.
Waheshimiwa Madiwani ,Viongozi wa dini , Viongozi wa Chama cha Mapinduzi ,watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Dua na Maombi ya kuliombea Taifa katika Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sapanjo Wilaya ya Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.