Toka tumeanza kukagua na kutembelea Miradi hakuna miradi iliyoenda vizuri kama hapa Chunya.
Hayo yamebainiwa wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi [CCM] Mkoa wa Mbeya walipo tembelea na kukagua Miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaotekelezwa chini ya Mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko19.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Ndg Saad Kusilawe akisema anawapongeza viongozi na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa Usimamizi na Utekelezaji mzuri wa Ujenzi wa vyumba vya madarasa.
“Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa majengo haya kwani ukitamzama yanaakisi kiwango cha fedha zilizotolewa, mmefanya vitu vizuri sisi kama CCM mkoa tumeridhishwa na hiki tulicho kiona” Kusilawe
Pia Kusilawe aliongeza kwa kusema wao kama CCM Mkoa wameridhishwa na miradi yote waliotembelea na hakuna hata mradi wowote wenye tatizo nao wameridhika, viongozi endeleeni kufanya kazi na muwe na ushirikino kwani ni jambo la msingi sana.
Naye katibu wa Itikadi siasa na Uenezi mkoa wa Mbeya Ndg Bashiru Madodi amesema Chama cha Mapinduzi mkoa wa mbeya kimeridhika na kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wilaya ya Chunya, niwapongeze Viongozi wote wa halmashauri hii kwa kazi kubwa na Nzuri ya Ujenzi wa Madarasa.
“Toka tumeanza kukagua na kutembelea miradi hii hakuna miradi iliyoenda vizuri kama hapa halmashauri ya wilaya ya Chunya, kazi ya ujenzi wa madarasa wilaya ya chunya CCM mkoa tumeridhika nayo”.
Katika ziara ya CCM mkoa miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa vyuma vya madarasa shule ya sekondari Isanyela, Shule ya Sekondari Kiwanja, Shule ya Sekondari Makongolosi, Kituo shikizi cha Kalungu na Kituo shikizi cha Machinjoni.
Wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya wakikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Kituo shikizi Cha Kalungu
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.