Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuanza kusikiliza rufaa zilizokatwa na wagombea wa ngazi za ubunge na udiwani kutoka majimboni ambapo hadi sasa tayari imepokea rufaa 557.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocle Kaijage amesema rufaa hizo zimetokana na baadhi ya wagombea ubunge na udiwani kutoridhika na maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi .
“Hadi sasa NEC imepokea rufaa zipatazo 557 ambazo tutaanza kuzifanyia kazi na tutajitahidi kuzitolea uamuzi mapema kwa kadri itakavyowezekana,”amesema.
Wakati huo huo NEC imetoa wito kwa makundi mbalimbali kuendelea kuheshimu sheria za uchaguzi zilizowekwa ili kuhakikisha kila raia mwenye haki ya kupiga kura wanatimiza wajibu wao kikatiba.
“Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977 imeweka masharti ya wajibu wa mtu kufuata na kutii Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano ,” amesema Mhe.Kaijage.
Amesema vivyo hivyo ,Ibara hiyo imeainisha haki ya kila mtu, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria, kuchukua hatua za kisheria kwa madhumuni ya kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi.
Aidha Kaijage amesema kwa msingi huo, malalamiko ya ukiukwaji wa masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na Kanuni zilizotungwa chini ya Sheria hizo,yanapaswa kushughulikiwa.
Amesema malalamiko hayo yanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu kufuata taratibu zilizowekwa .
“Nitumie fursa hii kuwapongeza wagombea wa vyama vya Siasa ambao wamedai haki zao kwa kufuata taratibu za kisheria na za kikanuni katika kuweka pingamizi mbali mbali na hatimaye kukata rufaa NEC,” amesema Jaji Kaijage.
Jaji Kaijage amesema NEC yeye kama kiongozi watashughulikia rufaa zote kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.
CREDIT: MPEKUZIHURU.COM
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.