Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Chunya Mhe James Mhanusi amewataka wananchi wa Wilaya ya Chunya na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha wanashirikiana na Mhakama ili kuhakikisha haki ya mtu yeyote inapatikana kwa wakati ili kujenga jamii bora yenye kujaliana na hatimaye kuendelea kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 27/1/2023 alipoongozo timu ya wataalamu wa sheria walipokuwa wanatoa elimu ya sheria katika kata ya Lupa ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa Elimu sharia katika wiki ya Sheria ambayo ilianza rasmi tarehe 24/1/2024 na itatamatika tarehe 1/2/2024
“Tukishirkiana kwa pamoja tunaweza kuboresha haki jinai lakini mkituachia mahakama peke yake inapelekea kesi nyingine kufutwa kwakuwa tunakosa ushahidi hivyo jamii ya wanachunya na watanzania kwa ujumla tushirikiane, mje mtoe ushahidi pale panapobidi na kwakufanya hivyo tutakuwa tunaboresha upatikanaji wa haki”
Aidha Mhe Mhanusi amesema Mahakama sasa inatumia digitali katika hatua mbalimbali za uendeshaji wa Mashauri na uboreshaji huo umesaidia kuokoa muda wa mteja, kupunguza gharama za uendeshaji wa kesi kwa mteja lakini pia imepunguza umbali wa mwananchi kufuata huduma ya Mhakama kwani mwananchi anaweza kupata huduma za mahakama akiwa maeneo anayoishi
“Kwasasa mahakama inafanya shughuli zake kwa njia ya mtandao hivyo kupitia mtandao mnaweza kupata huduma mbalimbali za mahakama hata bila wewe kufika mahakamani hivyo kupitia njia hiyo tunaokoa muda wenu, fedha na hata kurahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama” Amesema Mhe Mhanusi
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata Elimu ya Sheria wameshukuru sana wiki ya Sheria kufunguliwa rasmi kata ya Lupa kwani kupitia wiki hiyo elimu ya sheria imetolewa huku sula la Mirathi, migororo ya ardhi ikiwa na nafasi kubwa katika maswali ya wananchi hao
Maadhimisho ya wiki ya sheria huadhimishwa kila mwaka nchini Tanzania ambapo kwa mwaka huu Mahakama wilayani Chunya imezinduliwa rasmi leo tarehe 27/1/2024 kwa wananchi wa kata ya Lupa na kupatiwa Elimu juu ya mausuala ya Mahakama na Sheria kwa ujumla, wakati taehe 29/1/2024 timu ya uelimishaji itakuwa Shule ya Sekondari Itewe na baadaye Hillland,Tarehe 30/1/2024 itakuwa zamu ya Kiwanja na Isenyela Sekondari, tarehe 31/1/2024 itakuwa ni zamu ya Gereza la Chunya na Shule ya Sekondari Chokaa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Chunya Mhe James Mhanusi akiwa anawasilisha mada wakati wa ufunguzi wa wiki ya Sheria ambapo wilaya ya Chunya wamefanya ufunguzi rasmi leo katika kata ya Lupa
Moja ya watoa mada wakati wa ufunguzi rasmi wa wiki ya Sheria wakati akiwasilisha mada kwa wananachi waliojitokezo viwanja vya ofisi ya kijiji cha Ifuma, kata ya Lupa mapema leo
Afisa tarafa wa Tarafa ya Kipembawe ndugu Kassim Salum Kirondomara akizungumza jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa wiki ya Sheria Mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.