Katibu tawala wa wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero akimwakilisha mkuu wa wilaya katika maadhimisho ya siku ya kumbukizi ya mMashujaa amewaasa wananchi wa wilaya ya Chunya kuilinda Amani tuliyonayo kwani Amani hainunuliwi kama bidhaaa nyingine tukiipoteza Amani kuirejesha ni kazi kubwa hivyo twendelee kuilinda na kuidumisha Amani ya nchi yetu
Hayo ameyazugumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukizi ya mashujaa waliopigania taifa letu ambayo huadhimishwa julai 25 kila mwaka ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Chunya Maadhimisho hayo yamefanyika leo 24/07/2023 katika soko la Uhindilini lililopo kijiji cha Kibaoni kata ya Chokaa.
“Tunapaswa kuwaenzi mashujaa wetu kwa vitendo kwa kuilinda Amani tuliyonayo jukumu la kuilinda Amani ni suala la kila mmoja wetu si suala la viongozi au chama fulani tukumbuke kwamba Amani ikitoweka haitaangalia kiongozi au kada wa chama fulani kwahiyo tuilinde sana Amani yetu tuliyonayo” amesema Michombero
Akisoma taarifa ya siku ya mashujaa ndugu Anakleth Michombero amesema kuwa tuna adhimisha siku hii kwa kuwakumbuka mashujaa waliojitoa uhai wao kupigania taifa letu kwa Uzalendo Kama Halmashauri ya wilaya ya Chunya tunaungana na Taifa kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wetu walipoteza maisha yao wakati wakuipigania nchi yetu kwa kuidumisha na kuiendeleza misingi ya Amani waliyotuachia.
“Misingi mizuri na amani iliyojengwa na waasisi wa Nchi yetu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati Abeid Amani Karume imetufanya wananchi wa Chunya kuishi kwa Amani na utulivu huku tukifanya shughuli zetu za kila siku za maendeleo bila kubuguziwa na kuingiliwa na mtu yeyote hali ambayo imesababisha wilaya yetu ya Chunya kuwa kivutio kizuri cha uwekezaji katika shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini, kilimo cha mazao mbalimbali na Ufugaji”
Akitoa salamu katika maadhimisho hayo Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya ndugu Charles Jokery Amesema kuwa Nchi hii imepiganiwa na watu wengi kutoka sehemu tofauti tofauti za nchi yetu Akiwemo hayati mwalim Julius Kambarage Nyerere ,Hayati Abeid Amani Karume , na wengine wengi ambao leo hii wametufanya tunaishi kwa Amani na utulivu.
Awali akifungua maadhimisho hayo mwenyekiti wa kjiji cha kibaoni Ndugu Joshua Mambalala ameendelea kuwakumbusha wananchi kuhusu suala la usafi kuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku hivyo wananchi wanapaswa kuhakkikisha mazingira yanakuwa safi muda wote bila kusubiri msukumo kutoka kwa viongozi kila mtu anajukumu la kufanya usafi mazingira yanayomzunguka na kuhakiksha yanakuwa safi na salama muda wote kwaajili ya usalama wa afya zetu.
‘’Ndugu zangu niwaombe suala la usafi tusisubiri msukumo kutoka kwa viongozi wetu wa serikali usafi uwe sehemu ya maisha yetu ya kila siku tuhakikishe mazingira yetu yote yanakuwa safi na salama muda wote na kuifanya Tanzania yetu kuwa na mazingira safi na salama kwa afya zetu’’
Maadhimisho hayo ya kumbukizi ya siku ya mashujaa yameadhimishwa wilayani Chunya kwa kufanya usafi maeneo mbalimmali ya soko la uhindini, ikitanguliwa na dua ya kuwaombea mashujaa wetu iliyoongozwa na viongozi wa dini. Viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wilaya ya Chunya wamehudhuria,viongoziwa ulinzi na usalama, wafanyakazi halmashauri ya wilaya ya Chunya, wafanya biashara na wananchi wengine
Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya wakifanya usafi wa mazingira katika Soko la Uhindini siku ya maadhimisho ya kumbukizi ya mashujaa
Maafisa waJeshi la polisi wakifanya usafi wa mazingira siku ya kumbukizi ya Mashujaa katika Soko la Uhindini Wanafunzi wa shule ya msingi kibaoni wakifanya usafi wa mazingira katika Soko la Uhindini siku ya maadhimisho ya kumbukizi ya Mashujaa
Maafisa waJeshi la polisi pamoja na wananchi wakimsikiliza mgeni rasmi baada ya zoezi la usafi kukamilika
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.