Kaimu mwenyekiti wa Wadau wa Tumbaku Mkoa wa Kitumbaku Chunya Ndugu Lameck John Matukulu amewataka wadau na wataalamu wote wa tumbaku waliokusanyika wilayani Chunya kwa lengo la kufanya tathimini ya zao la Tumbaku kwa msimu huu wa 2023/2024 kuhakikisha wanatumia nguvu, akili na kujituma ili kuhakikisha matokeo ya zoezi la tathimini ya zao yanakuwa na uhalisia
Ametoa kauli hiyo tarehe 04/03/2024 wakati wa kikao cha kujengeana uwezo ikiwa ni maandalizi ya zoezi la kufanya tathimini ya zao la Tumbaku kwa msimu wa kilimo 2023/2024 zoezi ambalo linaanza rasmi tarehe 05/03/2024 zoezi ambalo litadumu zaidi ya siku 10 na litahusisha vyama vyote 33 vilivyopo katika Mkoa wa Kitumbaku Chunya
Awali akizungumza kuhusu tathimini ya zao hilo kwa msimu wa 2022/2023 katibu wa wadau wa Tumbaku mkoa wa kitumbaku Chunya ndugu Faustine Mtweve amewapongeza wajumbe walioshiriki zoezi la tathimini kwa msimu uliopita kwakufanya kazi kwa weledi kupelekea Mkoa wa Kitumbaku Chunya kuwa na ufanisi wa asilimia 101 jambo ambalo lilichagizwa na kujituma, uzalendo pamoja na ushirikiano uliokuwepo wakati wa zaoezi hilo hivyo amewataka wajumbe wa kikao kuhakikisha ufanisi unaongezeka Zaidi
“Mwaka jana tulifanikiwa kuwa na asilimia 101 za ufanisi hivyo lazima niwapongeze wote mlioshiriki zoezi la Tathimini msimu uliopita lakini niwaombe tushirikiane, tupendane na tushikamane ili kwa msimu huu tuwe na asilimia Zaidi ya tulizopata msimu uliopita na hilo linawezekana kama tukishirikiana bila kujali utofauti wa taasisi tunazotoka”
Naye Mjumbe mwezeshaji kutoka Bodi ya Tumbaku Mkoa wa Kitumbaku Chunya Ndugu Cleophas Nziku amewaambia wajumbe kwamba wanategemewa sana na taasisi walizotoka, serikali, wadau wa Tumbaku, Taasisi za kifedha na maeneo mengine hivyowameaasa wafanyekazi kwa weledi mkubwa ili wadau wote wanaowategemea wapate taarifa sahihi
“Takwimu hizi ni muhimu sana maana zinatumika maeneo mbalimbali ikiwemo Taasisi Binafsi na serikali wanategemea Takwimu hizi, Taasisi za kifedha na taasisi nyingine nyingi zinategemea takwimu zitakazopatikana kwenye tathimini ya zao la Tumbaku tunayotaraji kuaianza kehso hivyo nimwaombe tuwe makini sana. Sisi ni wataalamu na tunategemewa sana na tusifanye kazi kwa Mihemko, tuzingatie weledi ili tupate takwimu stahiki.
Akichangia mjadala wa utangulizi kabla ya kuanza rasmi zoezi la Tathimini Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kwawa Ndugu Goodluck Mwasa amewataka viongozi kuwa na uongozi mzuri na shirikishi kama walivyofanya msimu uliopita jambo lililopelekea Mkoa wa Kiumbaku Chunya kuwa na ufanisi mzuri wa asilimia 101
Naye Bwana Shamba ambaye pia ni meneja wa eneo kutoka Kampuni ya Premium Active ndugu Samwel J Philipo amewahimiza wadau wengine watakaoshirikiana kufanya tathimini ya zao la Tumbaku kwa mwaka 2024 kufanya kazi kwa bidii huku akiwakumbusha kuuliza maeneo yote korofi mapema wakati wa mafunzo hayo kwani kazi ya tathimi huwa inakuwa ngumu sana mnapoanza kufanyakazi ya kuathimini ili hali wengine bado kuna maeneo hawaelei nini cha kufanya
Zoezi la Tathimini ya zao la Tumbaku linalenga kupata makadirio ya uzalishaji wa zao husika kwa msimu wa kilimo mwaka husika ili maandalizi ya soko yaandaliwe sawa na makadirio husika, zoezi hilo linahusisha taasisi mbalimbali zikiwepo Halmashauri ya wilaya ya Chunya na Songwe, Bodi ya Tumbaku, Chama kikuu cha Ushirika wa wakulima wa Tumbaku Mkoa wa kitumbaku Chunya Mkoani Mbeya CHUTCU, Kampuni ya za unuazi wa Tumbaku ikiwa ni pamoja na Mkwawa, Premium, Magefa, Yaya, PATL Pamoja na TORITA/TARI
Wataalamu wa kilimo wakiwa katika tathimini kwa vitendo wakati wa kikao cha ufunguzi kilichoketi tarehe 4/3/2024
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.