Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi. Sophia J. Kumbuli ametoa eneo la hekari mbili (2) kwa ajili ya ujenzi wa ghala na soko la madini katika kata ya Mbugani kijiji cha Kiwanja.
Hata hivyo kutokana na kauli ya Mhe. Rais ya .... imeonekana kuwa zoezi hilo ni la haraka na mipango ya ujenzi soko hilo ni ya muda mrefu. Katika kulifanikisha zoezi hilo,Mkuu wa wilaya Mhe. Maryprisca Mahundi amefanya maongezi na uongozi wa benki ya NMB kwa ajili ya mpango wa haraka ambapo wamekubaliana kuwa, kwa sasa soko, pamoja na ghala litakuwa katika Tawi la benki ya NMB -Chunya kwani jengo hilo lina miundombinu rafiki.
Akiwa katika mkutano wa baraza la madiwani mwishoni mwa mwezi, hususani wakati wa kujadili agenda ya rasimu ya masoko ya madini, kwa pamoja Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Chunya wamefafanua ni namna gani soko la madini litafanikiwa likijengwa karibu na maeneo ya uchimbaji.
" Halmashauri itaongeza mapato yake kwa sababu watu watauza madini ndani ya halmashauri kitu ambacho kitaipatia halmashauri tozo na kodi mbalimbali. Pia itasaidia kuongeza usalama kwa wachimbaji kwani hawatatembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta soko. Soko hili pia litazuia utoroshaji wa madini kwani hakutakuwa na sababu ya kwenda mbali kuuza jambo ambalo litarahisisha mamlaka husika kufuatilia kwa ukaribu utoroshwaji wa madini". Mahundi.
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chunya amesisitiza sana kuhusu ukusanyaji wa mapato kwani mapato ni kipaumbele cha Taifa. Pia ameagiza timu ya mapato kuongeza jitihada katika makusanyo ya mapato, na kuahidi kuwa atahakikisha anaiwezesha timu ya mapato ili ifanye kazi kwa weledi na kufikia lengo la kukusanya zaidi ya 80% ifikapo mwisho wa mwaka
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.