Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imeibuka mshindi katika mashindano ya Afya na Usafi wa mazingira ambayo huratibiwa na Wizara ya Afya ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka nchi nzima katika mashindano yaliyofanyika Julai 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya Halmashauri za Wilaya 6 zinazopatikana katika Mkoa wa Mbeya
Takwimu hizo zinathibitishwa na ripoti ya matokeo ya Mashindano ya Afya na usafi wa mazingira mwaka 2023 yaliyotolewa na Wizara ya Afya ambapo zoezi hilo lilifanyika Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeshika nafasi ya 22 kati ya Halmashauri 137 zilizoshiriki wakati katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya Chunya Ndio Kinara kwa kushika nafasi ya kwanza, huku Kijiji cha Chunya Mjini kikishika nafasi ya 14 katika ya vijiji 274 viilivyoshiriki na kwenye Mkoa wa Mbeya Kijiji cha Chunya mjini Kimeshika nafasi ya kwanza kwa vijiji vyote vilivyoshiriki.
Afisa Afya wilaya ya Chunya ndugu Baraka Kipesha akiweka bayana baadhi ya mambo ambayo yamesababisha Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuibuka mshindi ikiwa ni pamoja na Ushirikiano na kujituma katika kazi lakini pia ufuatiliaji unaofanyika mara kwa mara na uhamasishaji juu ya usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya hadi kijiji
“Tumekuwa tukifanya ufuatiliaji na kuhamasisha juu ya usafi wa mazingira mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya vijiji na kaya katika Halmashauri yetu ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa Afya ya Wananchunya na kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya Afya na usafi wa mazingira kwani lengo letu ni kuwa nafasi ya kwanza kitaifa” alisema Kipesha
Aidha agenda ya usafi wa mazingira imekuwa ni agenda ya kudumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ili kuhakikisha jamii inaishi katika mazingira safi na salama pamoja na kujikinga na Magonjwa ya mlipuko ambayo husababishwa na uchafu wa mazingira ambapo katika ngazi za vijiji kumekuwa na sheria ndogo zinazotumika katika kusimamia usafi wa mazingira katika jamii.
Katika taasisi mbalimbali kama Shule kumekuwa na klabu za Usafi wa mazingira (School water sanitation and hygiene club) ambazo zimekuwa na jukuma la kuhamashisha wanafunzi wenzao kuzingatia usafi wanapokuwa shuleni na majumbani kwao ili kuweza kujiepusha na magonjwa ya mlipuko
Mashindano ya Afya na usafi wa mazingira ambayo hufanyika kila mwaka hujumuisisha maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi mbalimbali kama Hospitali , Kanisa , Mahakama Shule na maeneo mengine lakini pia kaya mbalimbali ambapo maeneo mbalimali hukaguliwa kulingana na vigezo vilivyoainishwa katika mwongozo ambapo kijiji cha Chunya mjini kimeibuka na Ushindi kwa kupata alama 179 kati ya alama 193 ambazo ni sawa na asilimia 93.
Ukitaka kuona taarifa kwa Undani Bonyeza link ifuatayo https://chunyadc.go.tz/announcement/matokeo-ya-mashindano-ya-afya-na-usafi-wa-mazingira-kitaifa-chunya-yafanya-vizuri
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.