Shughuli za uchimbaji madini zilizokuwa zikifanyika katika mto Zila uliopo kata ya Ifumbo Wilayani Chunya zimesimamishwa mpaka pale tamko lingine litakapotolewa na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde, na kwa yeyote atakae fanya shughuli yoyote katika mto Zila hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali za na zake pamoja na kuchukuliwa hatua zingine za kisheria.
Katazo hilo limetolewa leo tarehe 14/2/2025 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero ikiwa ni maelekezo kutoka kwa Waziri wa Madini mpaka pale yatakapo tolewa maelekezo mengine.
“Kuanzia leo tarehe 14/2/2025 shughuli zote za uchimbaji ndani ya mto zila zinasimamishwa rasmi kwa kampuni ya G.&I Mining Company Limited na kwa mtu mmoja mmoja mpaka pale waziri mwenye dhamana atakapo toa maelekezio mengine , kwamana hiyo serikali zote za vijiji , kijiji cha ifumbo na kijiji cha Lupamaketi tunatakiwa tusimamie zoezi hili.”amesema Michombero
Aidha amewaagiza wenyeviti wa vijiji vyote viwili , kijiji cha Ifumbo na Kijiji cha Lupamaketi kuhakikisha wanaitisha mikutano yay a hadhara katika vijiji vyao kwaajili ya kuwajulisha wananchi wao juu ya katazo hilo la kufanya kazi za uchimbaji au shughuli zozote katika mto zila mpaka pale watakapo pokea maelekezo mengine.
Nae Mwenyekiti wa Ifumbo ndugu Bahati Sinkwembe kwaniaba ya Wananchi amekiri kuyapokea maelekezo hayo kwaajili ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kufanya mkutano na wanakijiji kuwajulisha juu ya kutokufanya shughuli yoyote ndani yam to zila kwa masilahi ya wanaifumbo Wilaya ya Chunya na Taifa kwa ujumla.
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wengine ndugu Ephrahim Angolile , Erasto Waya na Frank Tewa wameuliza maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujua nani atakae simamia tamko hilo lakini pia kujua hatima ya maeneo ya wananchi yaliyoathiriwa na mwekezaji ambapo maswali yote yaliyoulizwa yalipatiwa majibu papo hapo.
Tamko hilo limetolewa mbele ya kamati ya Usalama Wilaya NEMC, Afisa Mazingira wa Wilaya ya Chunya, Afisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Chunya na Maafisa wengine kutoka Ofisi ya Madini, viongozi wa vijiji na wananchi wa kijiji cha Ifumbo na Lupamaketi, Katazo hilo limeenda sambamba na katazo alilolitoa Waziri wa Madini Mhe.Antony Mavunde wakati alipofanya ziara yake katika mto zila mwishoni mwa mwezi Desemba 2024.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero akitoa tamko kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Madini juu ya uchimbaji wa madini katika mto Zila uliopo kata ya Ifumbo Wilayani Chunya
Mwenyekiti wa kijiji cha Ifumbo ndugu Bahati Sinkwembe akikiri kupokea agizo hilo kwaajili ya utekelezaji .
Frank Tewa Mkazi wa kijiji cha Ifumbo akiuliza swali juu ya tamko lililotolewa kuhusu kutokufanya shughuli yoyote ya uchimbaji katika mto zila uliopo kata ya Ifumbo Wilayani Chunya.
Wananchi wa kijiji cha Ifumbo na Lupamarket wakisikiliza maelekezo yanayotolewa na katibu Tawala Ndugu Anakleth Michombero kuhusu Mto zila.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.