Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Deutsche Stiftung Wettbevolkerung (DSW), Peter Owaga ametambulisha mradi wa Reproductive Equity Strategy in Tanzania - REST, ambao utajikita katika upatikanaji na utumiaji wa huduma za afya na elimu ya uzazi, kujikinga na mimba za utotoni, VVU, kutokomeza ukatili kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mradi wa REST, Mkurugenzi wa DSW, Peter Owaga Novemba 22, 2024 katika Ukumbi wa Ofisi ya DSW uliopo Mbeya mjini amesema mradi wa REST utafika kwenye kata sita zilizopo Wilaya ya Chunya ambazo ni Kata ya Sangambi,Chokaa, Matundasi, Makongolosi, Lupa na Mafyeko ili kukutana na watendaji kata na maafisa maendeleo ya jamii ili kutoa elimu na uelewa kuhusu mradi wa REST ambao malengo yake ni kutoa elimu ya afya ya uzazi,kujikinga na mimba za utotoni, VVU, kutokomeza ukatili kwa wananchi wa Wilaya ya Chunya.
“Tunatarajia kufika Chunya tarehe 1 Disemba, 2024 siku ya maadhimisho ya UKIMWI duniani ambapo tutakutana na viongozi wa kata sita tulizozichagua ili tuwape uelewa kuhusu mradi na namna ya kuutekeleza ili kujenga ustawi wa jamii bora kwa wananchi wa Chunya” amesema Owaga.
Kwa upande wake mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya Dkt. Darison Andrew amesema watafanya tathmini ya utekelezaji wa malengo ya mradi ili kuona mabadiliko ambayo yatasaidia kuleta tija ya mradi kama ulivyopangwa.
“Natamani kuona kuimarika kwa ushiriki, kuongezeka kwa uwezo wa wadau, kuanzishwa kwa Klabu za Afya shuleni, kuwezesha vijana kutambua afya zao kupitia Klabu za Afya ili kujenga jamii bora na kupata tathimini ya tija ya mradi” amesema Dkt. Darison.
Naye, Bi Ester Kondobole, kaimu Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Chunya amesema mradi wa REST umefika wakati muwafaka Chunya ambapo utasaidia kuleta matokeo chanya na kuboresha afya kwa jamii ya wananchi wa Chunya.
Shirika la DSW linatekeleza mradi wa REST kwa lengo la kutoa elimu ya afya na maendeleo katika kwa jamii katika mikoa sita ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Iringa, Arusha na Mbeya. Katika Mkoa wa Mbeya Shirika litatekeleza mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
b
Baadhi ya Washiriki wakifuatikia kwa ukaribu kikao cha utambulisho wa mradi wa REST uliofanyika kwenye ukumbi wa shirika la DSW, Mkoa wa Mbeya leo 22 Novemba, 2024
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.