Mkurugenzi msaidizi Elimu anayesimamia elimu ya awali na Msingi Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwalimu Suzana Nussu amesema Serikali ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamilia kurudisha hadhi, heshima na thamani ya walimu nchini Tanzania Jambo ambalo litapelekea kufanya kazi kwa kujituma na kwa kujiamini wawapo katika kutekeleza majukumu yao na kwa kufanya hivyo itaongeza ubora wa Elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi wanapohitimu ngazi mbalimbali za Shule.
Ametoa kauli hiyo Leo tarehe 31/5/2024 wakati akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) mbele ya walimu kutoka Idara ya elimu awali na msingi pamoja na walimu kutoka idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake baada ya kuhitimisha ziara kama hiyo Mkoa wa Songwe.
“Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) tunataka hadhi, heshima na haki ya Mwalimu irudi. Hatuwezi kutekeleza hayo kwa kukaa ofisini hivyo ofisi nzima imegawanyika Nchi nzima kuongea na walimu kuhusu hilo lakini pia kutoa mrejesho wa mambo mbalimbali ambayo yanaendelea kutekelezwa na Serikali ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ili kurudisha hadhi ya mwalimu. Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema tuwambie anawapenda sana’’ amesema Mwalimu Nussu
Aidha, Mwalimu Nussu amewathibitishia walimu wa wilaya ya Chunya kwamba kuanzia Mwezi Januari walimu wameendelea kulipwa madai yao huku akisema zaidi ya walimu 100 (104 walimu kutoka idara ya Elimu ya awali na Msingi, walimu 15 kutoka Idara ya Elimu Sekondari) watapandishwa madaraja kwa mseleleko kwenda Daraja wanalostahili baada ya takwimu kuonesha wanalipwa mishara ambayo sio ya daraja analostahili kuwepo
Naye Afisa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mwalimu Liliani Nyinge amewakumbusha walimu waliohudhuria kikao hicho kwamba wanapotekeleza majukumu yao wakumbuke kuzingatia uwezo wa mtoto mmoja mmoja kwanza, utayari wa mtoto huyo kujifunza, umri wake, pamoja na mazingira anayotoka. Mambo hayo manne kwa pamoja yakizingatiwa yanaweza kusaidia kuamua njia sahihi ya kuwasaidia wanafunzi hao na wakapata matokeo sahihi hatimaye kuwa msaada kwa familia zao hapo baadaye.
Awali akitoa taarifa ya Elimu katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Afisa Elimu awali na Msingi Mwalimu Ferd Y. Mhanze amesema, Halmashauri ya wilaya ya Chunya imenufaika sana na Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwakuipangia walimu wengi wilaya hiyo, tofauti na utaratibu wa kupanga watumishi uliokuwa unatumiwa hapo awali, Hivyo ameomba matumizi ya mfumo huo maalumu wa kuwapangia walimu vituo vya kazi uendelee ili Wilaya ya Chunya iendelee kunufaika zaidi na hatimaye lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuwahudumia wananchi wake kwa kuwapatia Elimu bora litimie Chunya.
“Tunawashukuru TAMISEMI kwa kutumia mfumo maalumu kugawa walimu, kwani wilaya ya Chunya tumepata walimu wengi tofauti na ilivyokuwa hapo awali hivyo ni maombi yetu matumizi ya Mfumo huo wa kuwapanga walimu uendelee ili wilaya ya Chunya tuendelee kupata walimu wengi zaidi na kwakuwa tunashukuru na kushukuru ni namna nyingine ya kuomba hivyo tunaomba muendelee kuitazama Chunya kama mnavyoitazama sasa” Amesema Mwalimu Mhanze
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu Hamis M. Mapato kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Chunya amesema Halmashauri ya wilaya ya Chunya inafanikiwa kutekeleza vigezo vyote vya upimaji kutokana na ushirikiano mzuri pamoja na uwajibikaji wa walimu kutoka idara zote za Elimu Msingi na Sekondari.
“Mafanikio yaliyosomwa hapa katika taarifa ya Idara za Elimu ya awali na Msingi na Taarifa ya Idara ya Elimu Sekondari yamechagizwa na walimu hawa walioko mbele yako, Tumepita kwenye vituo vyao kuwahimiza kulingana na Vigezo vya upimaji wa ufaulu (Key Perfomrmance indicators KPI). Ndugu washiriki wa kikao hiki tunao ugeni wa Kitaifa umekuja kushuhudia namna tulivyo tekeleza vigezo vya KPI naomba kuwasihi na kuwaomba tusikilize na tumfuatile ili tupate lengo la Serikali kwetu” Amesema Mwalim Mapoto.
Kikao hicho kimehusisha walimu zaidi ya mia tatu na hamsini kutoka idara ya elimu ya awali na msingi, pamoja na idara ya elimu ya Sekondari wilaya ya Chunya, walimu wakuu, wakuu wa shule maafisa Elimu kata na watumishi wa idara za Elimu awali na msingi, idara za elimu sekondari, Idara ya Utumishi, Tume ya utumishi wa walimu (TSC) Ofisi ya Mdhibiti ubora sambamba na ugeni kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI
Afisa Elimu Sekondari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalim Hamis M Mapoto akizungumza wakati wa kikao cha walimu mbele ya viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI mapema leo kwenye ukumbi wa Mikutano Sapanjo
Afisa Elimu awali na Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya akiwasilisha Taarifa ya Elimu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mbele ya walimu na wagenzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI leo katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Baadhi ya walimu kutoka Idara ya elimu awali na msingi pamoja na walimu kutoka Idara ya Elimu Sekondari ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakisikiza kwa makini maelekezo na Mafunzo kutoka Viongozi Ofisi ya Rais TAMISEMI mapema leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Mkurugenzi msaidizi Elimu anayesimamia elimu ya awali na Msingi Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwalimu Suzana Nussu akiendelea kuwasilisha namna ambavyo Serikali ya awamu ya sita inatekeleza mambo mbalimbali ili kurudisha hadhi na heshima ya Mwalimu nchini
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.